Kocha mkuu
wa Zamalek Helmy Tolan ameelezea kufurahishwa kwake na matokeo ya ushindi ya
magoli 2-1 dhidi ya Orlando Pitares wakati wa mchezo wao wa makundi ya ligi ya
mabingwa barani Afrika.
Tolan
amesema kuwa haikuwa kazi rahisi kwa wao kuchomoza na ushindi ukizingatia
wapinzani wao wanatimu nzuri zaidi ya kikosi cha Zamalek hata hivyo jitihada za
vijana wake zimewawezesha kuchomoza na alama 3 muhimu kunako mchezo huo.
Endapo
Zamalek wangepoteza mchezo huo ingekuwa ndiyo tiketi ya wao kuyaaga michuano
hiyo lakini ushindi wa magoli 2-1 unaibua matumaini mapya kwa kikosi hicho
kusonga mbele katika mechi zingine zilizosalia.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni