Jumatano, 18 Septemba 2013

ASHANTI UNITED YAMUANGUKIA KASEJA WAHITAJI SAINI YAKE KIBINAADAMU ZAIDI




Wauza mitumba wa ilala Un colonized never say die titi munda mtwale wa kuchwela watoto wa jiji Ashanti united wanakaba kayeka wameonesha nia ya kutaka kumsajili nahodha na mlinda mlango namba moja wa timu ya Taifa ya Tanzania Taifa stars Juma K Juma, Juma Kaseja.
Ashanti United inayodhaminiwa na kampuni ya S.S.B kupitia kinywaji chake cha Azam Malta kimetangaza dhamira hiyo kuelekea kwenye dirisha dogo la usajili ambalo linataraji kufunguliwa November 15 hadi Disemba 15 mwaka huu.

Katibu mkuu wa Ashanti Abubakar Silas amesema kuwa ndoto kubwa ya Ashanti ni kutaka kumsajili Juma Kaseja ambaye ni mchezo mkubwa hapa nchini mwenye uzoefu wa kutosha wakiamini atakuwa na msaada mkubwa kuiwezesha Ashanti kufanya vizuri kwenye msimu huu wa Ligi.
Silas amemtaka Kaseja kuwatazama Ashanti kwa jicho la tatu kwakuwa nib ado timu changa na haina uwezo wa kutosha kumsajili kwa dau kubwa litakaloendana na hadhi yake.

“Sisi kama Ashanti United kwa mtu kama Kaseja anaweza kusaidia sana siyo siri, kwa mazingira yaleyale tulomchukuwa Said Maulid tunaweza kumchukuwa Kaseja unajuwa katika mpira kila samaki ana price yake
 “Kaseja ni mchejazi mkubwa ni Tanzania one, price Tag yake ni kubwa sasa yeye binafsi kama alivyoonesha nia SMG na yeye afanye hivyo hivyo”
“Iwapo atakuwa tayari sisi tunamtaka Kaseja ijapokuwa hatuna pesa za kumlipa”
Kwa upande wake Juma K Juma amewatoa hofu Ashanti United pamoja na kuwataka wakae kwenye meza ya mazungumzo pamoja nae ili kufikia muafaka wa kuipata ridhaa yake kuitumia klabu hiyo kwenye msimu wa 2013/2014.

“Kwanza wanatakiwa wakae na mimi wasiniogope wanatakiwa kwanza waniite mimi tukae tuongee then wanisikie wanaweza wakawa wananiogopa kumbe ikawa tofauti na wanavyofikiria”

“Kuna timu ambazo unaweza kwenda kucheka tu kwa kujitolea timu kama Ashanti ni ya kujitolea kikubwa wakae na mimi wafanye maongezi bado nawapenda mashabiki wangu waendelee kunisupport Inshaallah Mola ataleta kheri yake.”

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni