Jumanne, 24 Septemba 2013

ASHANTI YAAHIDI POINTS 3 HAPO KESHO

Ligi kuu soka ya Tanzania bara inataraji kuunguruma tena hapo kesho kwa kushuhidiwa mchezo mmoja pekee utakaopigwa kwenye uwanja wa Ally Hassan Mwinyi mjini Tabora ambapo wenyeji wa Rhino Rangers watawakaribisha wauza mitumba wa Ilala watoto wa jiji Ashanti United.
 Timu zote zinashuka dimbani zikiwa tayari zimeshacheza mechi tano ambazo kwa upande wa wenyeji Rhino rangers zimewawezesha kuvuna points 4 baada ya kutoka sare michezo minne na kupoteza mmoja wakati kwa upande wa Ashanti yenyewe imepoteza michezo minne na kutoka sare mmoja uliowapa alama 1 pekee.
Afisa habari wa Ashanti United Rajab Marijan amesema kuwa kikosi chao kipo imara kuelekea kwenye mchezo huo licha ya kukabiliwa na majeruhi akiwemo mkongwe Said Maulid.
“Kiujumla kimaandalizi tuko vizuro japo tuna matatizo na wachezaji wawili na kwamujibu wa taarifa ya daktari, wachezaji hao hawatocheza kesho”.
“Mechi za mikoani nguvu ingawaje TFF wakae na kuangalia upya kutokana na aina ya viwanja tunavyokutana navyo pamoja na michezo tunayokutana nayo, michezo ya mikoani imejaa fitna na haiangalii usawa”
Marijan ameongezea kuwa bado wananafasi nzuri ya kupata matokeo mazuri katika mechi zake za nyumbani huku akilitaka shirikisho la mpira wa miguu nchini TFF kutazama upya viwanja mbalimbali vya mikoani ambavyo vinatumika katika ligi licha ya kuwa katika ubora unaotakiwa.
Tumejipanga kuhakikisha tunashinda dhidi ya Rhino na turudi tukashinde mechi za nyumbani, kulingana na matokeo ya ligi timu hazijapishana sana kwahiyo matokeo hayatushtui”.
Kwa upande wa Rhino Rangers yenyewe wamesema kuwa mchezo huo utatumika kuwapa alama tatu muhimu zitazowaweka katika nafasi nzuri kuelekea kwenye mechi zake zingine za mzunguko wa kwanza wa ligi.
Ligi hiyo itaendelea tena September 28, ambapo mabingwa watetezi Yanga Afrika baada ya kupoteza mchezo wake uliopita mbele ya Azam, wanataraji kuzichanga upya karata zao za kutetea ubingwa watakapoikabili Ruvu shooting katika mchezo utakaopigwa uwanja wa taifa jijini Dar es salaam.
Huko Tanga katika uwanja wa Mkwakwani Mgambo JKT watamenyama na JKT Oljoro, Mbeya City wakiwakaribisha wagosi wa kaya Coastal Union katika uwanja wa Sokoine mjini humo huku Rhino rangers ikitaraji kujitupa tena kiwanja chake cha nyumbani kucheza dhidi ya Kagera sugar.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni