Jumanne, 24 Septemba 2013

TIMESOFMONEY YADHAMIRIA KUINGI KATIKA SOKO LA TANZANIA

24/09/2013: KAMPUNI kubwa duniani yenye utaalamu wa kuwezesha uhamisho wa fedha kwa njia ya mtandao (online) ya Timesof Money, imedhamiria kuingia katika soko la Tanzania, kama sehemu ya mpango wake wa upanuzi barani Afrika.
Katika mpango wake huo, kampuni hii yenye makao yake makuu jijini Mumbai nchini India, inatajaria kuzindua mpango/mfumo wa kutuma fedha nchini toka kwa Watanzania walioko nje ya nchi (remittance) kwa njia ya mtandao (Online).  Mfumo huo ambao unatarajiwa kuleta mapinduzi makubwa nchini, utawawezesha Watanzania kupata/kutuma fedha kutoka mahali popote duniani moja kwa moja katika akaunti zao za benki, kadi za malipo ya kabla (pre-paid cards) pamoja na simu zao za mkononi.
“Katika mkakati huo huo wa kijitanua barani Africa, hivi karibuni tumeingia mkataba na Benki ya Diamond Trust nchini Kenya kutoa huduma kwa wateja wake wa mfumo wa ‘NationHela’,” alisema Afisa Mtendaji mkuu wa TimesofMoney, Avijit Nanda.
Kwa mujibu wa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Tanzania, idadi ya Watanzania wanaoishi na kufanya kazi nchi mbalimbali duniani/ughaibuni (diaspora) inakadiriwa kuwa zaidi ya million mbili. Na kwa mujibu wa ripoti ya Benki ya Dunia, inakadiriwa kuwa Watanzania hao waliingiza nchini kiasi cha shillingi billion 120 (US$ 75million)mwaka jana. Kwa kutumia huduma hii, Watanzania wanaoishi nje ya nchi wataweza kutuma pesa kwa jamaa na marafiki zao nyumbani, hivyo kuondoa usumbufu wa kusimama katika foleni kwa mawakala wa kuhamisha fedha.
"Idadi ya raia wa nchi za Afrika Mashariki na hasa Tanzania wanaoishi nje ya nchi zao inaendelea kuongezeka na hii ina maanisha uhitaji wa kutuma fedha nyumbani (remittance) pia unaongezeka. Ni kwa sababu hii tumeona kuna umuhumi wa kuingia katika soko hili. Tukiwa na teknolojia ya kisasa, tunatoa ahadi ya huduma bora kwa kutumia wataalamu wenye uzoefu mkubwa katika nyanja hii,” alisema Bw Nanda.
Bara la Afrika linakadiriwa kuwa na idadi ya watu zaidi ya million 30 wanaoishi nje ya nchi zao za asili. Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo-- International Fund for Agricultural Development (IFAD), unakadiria kwamba mwaka jana (2012) wahamiaji hao kwa pamoja wamechangia/ wametuma kiasi cha dola za marekani millioni 38.6 katika fedha kutoka nje, kwa familia na jamii zao nyumbani.
Hata hivyo, moja ya kikwazo kikubwa kwa ukuaji wa mtiririko kutuma fedha nyumbani (remittance) katika nchi za Afrika hasa zile zilizopo Kusini mwa jangwa la Sahara, ni gharama kubwa ya kutuma fedha. Wastani wa gharama ya kutuma fedha kwa Afrika ni karibu 12 % ya juu kuliko wastani wa kimataifa wa 8.96 % na karibu mara mbili ya gharama ya kutuma fedha kwa Asia ya Kusini.
"Gharama kubwa za ada zinazotozwa na makampuni na mawakala wa kuhamisha fedha barani Africa, imekuwa ni kikwazo na imeathiri mtiririko wa kuingiza fedha toka nje ya nchi. Mtumiaji wa mwisho ndiye anayeathirika na kubeba mzigo wa gharama/ada kwa kiasi kikubwa. Kwa kupitai mfumo wa mtandao (online-transactions) tunatarajia  inaweza kusaidia kupunguza gharama hizi kwa kiasi kikubwa, jambo ambalo litatao ahueni kubwa kwa mtumiaji wa mwisho,” bosi huyo wa TimesofMoney alisema.

Kuhusu TimesofMoney :
TimesofMoney ni  kampuni inayoongoza duniani kwa kufanya biashara  ya uhamisho wa fedha  kitaalamu. Kampuni hii inisifika kwa kufanya biashara  na wateja mbalimbali wakiwemo wa rejareja na kitaasisi duniani kote.
Ikiwa imeanzishwa mwaka 2000, TimesofMoney, inatoa ufumbuzi  wa mifumo ya malipo kwa wafanyabiashara.
Huduma zinatolewa duniani kote - kuwezesha uhamisho wa fedha watu kwenda kwenye nchi zao za nyumbani na kutoa huduma ya urahisi wa kutumia internet au simu.
Ikiwa na zaidi ya miaka 12 ya uzoefu, TimesofMoney inajivunia mahusiano mazuri na ya nguvu na wateja wake wakiwemo wale wa rejareja, kitaasisi na pia inaheshima na mafanikio makubwa katika sekta ya fedha kwa miaka kadhaa sasa.
Kampuni hii pia inajuvunia kuwa mbia mkubwa (kuwa na hisa kubwa) katika Mtandao wa Kimataifa, na ni kiongozi wa soko katika mfumo wa malipo. Inasimamiwa na timu ya wataalamu wenye uzoefu kutoka benki na historia nzuri ya fedha.
Maelezo zaidi zinapatikana kwenye tovuti ya kampuni www.timesofmoney.com .
Kwa maswali wasiliana na:
Lucy T. Ngongoseke | Tabasamu Public Relations | (Mobile) +255 754 602674 | lucy@tabasamupr.co.tz
Bhavin Shah | TimesofMoney | (Desk) + 91-22-3098 8491 | bhavins@timesofmoney.com
Mike Omuodo | H+K Strategies | (Mobile) + 254-720910146 | Mike.Omuodo@hkstrategies.co.ke


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni