Jumatatu, 2 Septemba 2013

MALAWI WAIWAHI NIGERIA





Timu ya taifa ya Malawi imetuma waangalizi wake nchini Nigeria kwaajili ya kufanya ukaguzi wa eneo watakalofikia timu hiyo kabla ya mchezo wao wa kuisaka tiketi ya kutinga fainali za kombe la dunia mwakani dhidi ya Nigeria

Katibu mkuu wa shirikisho la mpira wa miguu la Malawi FAM Sugo Nyirenda na mhasibu wake Christopher Mdolo tayari wameshawasili nchini Nigeria na wanaendelea na maandalizi kuelekea kwenye mchezo huo wa kundi F.



Malawi kwasasa wako nchini Botswana ambako kesho watajitupa dimbani kucheza dhidi ya wenyeji wao
 ikiwa ni mchezo wa kimataifa wa kujipima nguvu.


Matokeo yoyote ya ushindi kwa Malawi yataiwezesha timu hiyo kusonga kwenye hatua ya mtoano wakati sare ya aina yoyote ile itaifanya Nigeria ifuzu katika hatua ya tatu ya mtoano ya mchujo wa kombe la dunia.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni