Kocha mkuu wa Kenya The Harambee stars Adel Amrouche
amevunja ukimya na kwanza mara ya kwanza ameiomba serikali ya nchini humo kuisaidia
timu yake kuelekea kwenye mchezo wao wa wikiend hii.
The Harambee stars kwasasa ipo kambini ikijiwinda
dhidi ya Namibia katika mchezo wa kuisaka tiketi ya kushiriki fainali za kombe
la dunia mwakani.
Adel ameitaka serikali kuwapa ari wachezaji pamoja
na kujitolea muda wao mwingi kuwahamasisha wananchi kuipa nguvu timu yao ya
taifa.
Kocha huyo amewataka wadau wengine kujitokeza kutoa
ahadi katika kikosi hicho ambacho kinatawaliwa na wachezaji wenye umri chini ya
miaka 25.
FIFA DELAY
SENEGAL-UGANDA BY AN HOUR
Shirikisho la mpira wa miguu duniani FIFA limefanya
mabadiliko ya muda kwenye mchezo wa hapo kesho kati ya Senegal na Uganda ukiwa
ni mchezo wa mchujo wa kombe la dunia 2014.
Mechi hiyo itapigwa Marakesh nchini Morocco, kuanzia
majira ya saa 3 usiku kwa saa za Morocco badala ya saa 4.
Rais wa Shirikisho la soka la Uganda Edgar Watson
amethibitisha kupokea taarifa hizo kutoka FIFA hata hivyo hawajafafanuliwa
sababu za mabadiliko hayo.
Senegal wanaongoza Kundi J wakiwa na alama 9
wakifuatiwa na Uganda wenye alama 8.
BAFANA V ZIM SET FOR ORLANDO
Mchezo wa kimataifa wa kirafiki kati ya timu ya
taifa ya Afrika kusini Bafanabafana na Zimbabwe uliopangwa kupigwa September 10
mwaka huu, imebainika utaunguruma kwenye uwanja wa Orlando kuanzia saa mbili na
nusu usiku.
Uwanja wa Orlando ni miongoni mwa viwanja vizuri
vilivyopo kwenye jiji la Polokwane moja
kati ya miji maarufu nchini humo.
Kocha mkuu wa Bafanabafana Gordon Igesund
amefurahishwa na uteuzi wa kiwanja hiko akiamini ni moja kati ya viwanja vizuri
kutumika na timu yake ya taifa katika uandaaji wa mechi za kimataifa.
CHIPOLOPOLO HELD UP IN LUSAKA
Timu ya taifa ya Zambia wanachipolopolo usiku wa
kuamkia leo ilishindwa kukwea pipa kuelekea nchini Ghana kutokana na kuchelewa
kukamilisha taratibu za safari hiyo.
Shirikisho la soka la Zambia limethibitisha timu yao
kuwekewa vikwazo Afrika kusini ambako waliweka kambi kujiandaa na mchezo huo wa
hapo kesho katika dimba la Kumasi dhidi ya wenyeji wao Ghana The Black stars.
Mpaka tunaingia mitamboni kikosi hicho bado
hakijapewa kibali ya kusafiri kutoka bondeni Afrika kusini kuelekea nchini
Ghana, hata hivyo Shirikisho la Zambia limeahidi kufanya kila liwezekanalo
kuhakikisha suala hilo linamalizika usiku huu.
Msafara wa Zambia umejumuisha makipa watatu, mabeki
saba, viungo tisa na washambuliaji watano.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni