Binti wa kinigeria
Obabiyi Aishah Ajibola mwenye umri wa miaka 21, jana ametangazwa kuwa mshindi
wa shindano la Miss World Muslimah wa mwaka 2013 lililofanyika mjini
Jakarta,Indonesia.
Mabinti 20 kutoka
nchi sita ndio waliofanikiwa kuingia fainali ambapo washiriki wote walivaa
hijabu na mavazi yaliyostiri maungo yao. Baada ya kuonesha watazamaji na wasomi
wa kiislamu, jopo la majaji lilimchagua Obabiyi Aishah Ajibola kutoka Nigeria
kuwa mshindi. Vigezo vilivyotumika kumpata mshindi ni Ufasaha wa kusoma Qurani
na Maoni yao juu ya Uislamu katika Dunia ya kisasa.
Baada ya kusikia
jina lake kama mshindi Obabiyi Aishah Ajibola, alilia kwa furaha na
kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa yeye kuwa mshindi. “Jambo hili hasa si kushindana
bali sisi tunajaribu tu kuonesha Dunia kwamba Uislamu ni mzuri” alisema Aishah.
Eka Shanti ambaye
ndiye aliyeanzisha shindano hili miaka mitatu iliyopita, baada ya kupoteza kazi
yake ya utangazaji wa Televisheni kwa kukataa kuvua Hijabu akiwa anatangaza,
anasema, "Mwaka huu tumefanya makusudi lianze shindano letu kabla ya Miss
World ili kuonesha kwamba kuna jambo mbadala na mfano wa kuigwa kwa wanawake wa
kiislamu.
Shindano hili
lilianza mwaka 2011 likiwa na jina tofauti lilishirikisha waindonesia peke
yake. Shanti anasema baada vyombo vya habari kulinganisha na Miss World
tulibadilisha jina na tulikubali kuweka wagombea wa kigeni mwaka huu. Washiriki
wa nje ya Indonesia, walitoka nchi za Iran, Malaysia, Bangladesh, Brunei,
na Nigeria.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni