Jumamosi, 7 Septemba 2013

SABAH SALUM MUCHACHO SAWA NA ASIA IDARIOUS WA KHAMSIN

Anaitwa Sabah Salum Muchacho, moja kati ya nyimbo zake alizowahi kuimba, wimbo huu wa Tamba ni miongoni mwa nyimbo zisizochuja masikioni mwa wadau wa muziki huu wa Taarab.

Sabah Salum Muchacho
Kama umewahi kuwa katika mahusiano na kwa bahati mbaya mwenza wako akasafiri au mkawa mko mbali basi amini huu wimbo unakugusa .
Huyu mwanamama hachuji kwa sauti yake wala uzuri wake, Mashaallah Mwenyezi kamjaalia anajipenda kwa rangi, mavazi, umbo ndo usiseme.


Huwa namfananisha sana na Asia Idarious wa Khamsin mamaa Fabak Fashion, wote ni wanamama wanaojipenda kimuonekana na hawaringi abadan.
Asia Idarious Khamsin


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni