Jumanne, 3 Septemba 2013

KISIWA CHA SAANANE CHATANGAZWA RASMI HIFADHI YATAIFA



Kisiwa cha Saanane kimetangazwa rasmi kuwa Hifadhi ya Taifa kufuatia Tangazola Serikali Namba 227 lililotolewa hivi karibuni.Kutangazwa kwa Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Saanane kunafuatia kupitishwakwa Azimio la Bunge mwezi Oktoba mwaka jana lililoridhia kupandishwa hadhikwa kisiwa hicho kutoka Pori la Akiba na kuwa Hifadhi ya Taifa.

Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Saanane itakuwa na ukubwa wa kilomita za mraba2.18 na itajumuisha maeneo ya lililokuwa Pori la Akiba , Visiwa vya Chankendekubwa na ndogo pamoja na eneo la maji ya Ziwa Victoria linalozunguka visiwahivyo. 

Kuanzishwa kwa Hifadhi mpya ya Taifa ya Saanane kutawezesha haja yakuongeza spishi mbalimbali za wanyamapori na hivyo kuongeza utalii wa mjini,utalii wa ndani, utafiti na kutoa elimu kwa vitendo kwa wanafunzi na wananchiwatakaotembelea hifadhi hii mpya.Aidha, uamuzi huu utasaidia kutunza hali ya bioanuwai, uhifadhi wa mazalia namakuzio ya samaki na uendelezaji wa utalii wa mjini kuendelea kuimarika.

Kabla ya kupandishwa hadhi, Kisiwa cha Saanane kilikuwa Bustani ya wanyamamwaka 1964 kabla ya kupandishwa hadhi kuwa Pori la Akiba mwaka 1991.Ilipofika mwaka 2006, Serikali ilikikabidhi kisiwa hicho kwa Shirika la Hifadhi zaTaifa kwa ajili ya kukiendesha na kusimamia mchakato wa kukipandisha hadhikuwa Hifadhi ya Taifa.Kufuatia uamuzi huu, Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) sasa litakuwa na jumla ya Hifadhi 16 nchi nzima ambazo nyingine ni pamoja na Serengeti; ZiwaManyara; Tarangire na Arusha.


 Nyingine ni pamoja na Kilimanjaro; Mkomazi; Saadani; Mikumi; Milima yaUdzungwa; Ruaha; Kitulo; Katavi; Gombe; Milima ya Mahale na Kisiwa chaRubondo.

Wakati huohuo,

eneo la Hifadhi ya Taifa Gombe limeongezwa ukubwa kutokaKilometa za mraba 33.74 hadi kufikia kilometa za mraba 56. Uamuzi huuunatokana na Tangazo la Serikali Namba 228 lililotolewa hivi karibuni ambalolinafuatia Azimio la Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lililotolewamwaka jana linalohusu kuridhiwa kwa uamuzi wa kurekebisha mipaka ya Hifadhiya Taifa Gombe kwa kuondoa eneo la makaburi na kuliacha kwa wananchi pamoja na kujumuisha eneo la ufukwe wa maji ya Ziwa Victoria na eneo laukanda wa maji.

Kuongezeka kwa eneo la ufukwe wa ziwa na ukanda wa maji kwenye eneo lahifadhi kutaongeza wigo wa shughuli za utalii katika Hifadhi kama vile kuogelea,utalii wa boti, mitumbwi na uvuvi wa kitalii.

Imetolewa na Idara ya UhusianoHifadhi za Taifa TanzaniaS. L. P 3134ARUSHA

 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni