USAHIHI WA TAARIFA ZA MGENI ALIYEUWAWA NA TEMBO
NJEYA HIFADHI YA TARANGIRE
Baadhi ya vyombo vya habari nchini jana na leo
vimekuwa vikiripoti juuya tukio la kuuwawa na tembo kwa mgeni kutoka
Marekanianayefahamika kama Thomas Vardon Macfee (58) tarehe 31.08.2013
katikaHifadhi ya Taifa Tarangire.
Shirika la Hifadhi za Taifa linapenda kuweka
usahihi wa taarifazilizoripotiwa kama ifutavyo:-Tukio la mgeni husika lilitokea
nje ya Hifadhi ya Tarangire katika kijiji chaKakoi kambi ya Tarangire River
Camp, wakiwa wanafanya utalii wakutembea kwa miguu “Walking Safari”.
Baada ya
kuvamiwa nakuumizwa, mgeni huyu alifikishwa katika zahanati ya Hifadhi
yaTarangire na watumishi wa kambi aliyofikia iliyo nje ya hifadhi kwa ajiliya
matibabu ya huduma ya kwanza na alipofikishwa, alifariki dunia.Hivyo basi,
Shirika linapenda kusahihisha kuwa
tukio lililopelekea kifocha mgeni lilitokea nje ya
Hifadhi ya Tarangire na si ndani kamailivyoripotiwa.
IMETOLEWA NA
IDARA YA
UHUSIANO
HIFADHI ZA TAIFA
S.L.P 3134ARUSHA
05/09/2013
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni