Jumamosi, 14 Septemba 2013

WEMA SEPETU KUITWA MKE WA MTU


Anaitwa Wema Abraham Sepetu almaarufu Beautiful Onyinye amezaliwa September 28 mwaka 1988 na ni binti wa miwsho kati ya mabinti wanne wa balozi Abraham Sepetu.
Mali za Mzee Sepetu hizo "dada zake Wema"
Alianza kama mlimbwende aliyefanikiwa kutwaa taji la miss Tanzania mwaka 2006 na hapo ndipo uzuri wake, kipaji chake na elimu yake ikamfanya aingie kwenye tasnia ya filamu aliko ng'ara kwa mara ya kwanza akiwa na Marehemu Steven Kanumba kwenye movie ya Point of no Return.


Nabii hakubaliki kwao ila kwa Wema imekuwa tofauti wapo wanaosema wema kicheche, hajatulia wakatin huo huo wapo wanampenda Wema mimi nikiwa mmoja wao.

Penye wengi pana mengi Mwanadada huyu amekuwa akihusishwa na mahusiano ya kimapenzi na mastaa wengi nchini lakini katika yote penzi lake na Diamond ni funga kazi na funga mwaka, sijui kwanini wawili hawa waliachana wakati ukweli walikuwa wanapendana na naimani bado Wema anampenda sana Naseeb Abdul "Diamond".
Wema na Diamond
Mbali na Diamond wapo wengine wametajwa wakina Mr.Blue,Charlz Baba,Steven Kanumba ,james fredrick, Jumbe na wengine wengi, ingawaje kwa muda huu bado haijajulikana wazi ana mahusiano na nani.

Wema amekuwa mwepesi sana kuwasaidia watu mbalimbali wakiwemo wasanii wenzake, watoto ya yatima na kwa muonekano wake naamini Wema ana kila sababu ya kuwa mke wa mtu kwa sasa.

Wema akimnusuru Kajala kwenda jela

Mavazi ya Wema siku hizi ni tofauti na hapo awali, umapepe wa Wema haupo tena, Wema amekuwa amekuwa mkubwa, Wema amekuwa mama na kwanini Wema asiwe mke wa mtu?

Wema katika muonekana kama wa ndoa ila mambo ya maulid hayooooo
Wema akifutarisha

Wema my dear una kila sababu ya kuwadhihirishia watanzania kuwa sasa umebadilika hebu tutambulishe shemeji yenu na mkweee hehehheheheheheh we love u mamaaaaaaaaaaaaa
 
Onyine wa bongo
WEMA ANA KAMPUNI YAKE MWENYEWEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEE
sehemu ya ofisi ya Wema
Sehemu ya ofisi ya Wema
 
Wema ndani ya ofisi yake

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni