Jumamosi, 14 Septemba 2013

TANZANIA AIRTEL RISING STARS YAKABIDHIWA BENDERA




 
Kulia ni Boniface Wambura afisa habari wa TFF, katikati ni Angetile Osiah katibu mkuu TFF, na wa mwisho kushoto ni Jackson Mbando meneja uhusiano wa Airtel
Timu ya taifa ya Airtel rising stars ya Tanzania, leo imekabidhiwa bendera tayari kwa ajili ya safari ya kuelekea nchini Nigeria kushiriki mashindano ya dunia ya Airtel rising stars yatakayotimuvua vumbi September 16 mwaka huu.

Timu hiyo inayoundwa na wachezaji 32 waliopatikana kwenye kombaini za mikoa, 16 wakiwa ni wavulana na 16 wasichana wanataraji kuondoka kesho wakiwa na kauli mbiu ya kurejea nchini na ubingwa wenye thamani ya kitita Dola 10,000/= sawa na zaidi ya Millioni 16 kwa pesa ya Tanzania.
Katibu mkuu wa TFF Angetile Osiah akinena jambo

Meneja uhusiano wa kampuni ya simu za mkononi ya Airtel ambao ndiyo wadhamini wakuuwa michuano hiyo Jackson Mbando amewataka wachezaji kuwa na uelewa juu ya kile wanachokwenda kukifanya kwakuwa haya ni mashindano makubwa ya dunia na jukumu lao kubwa ni kuhakikisha wanarejea nyumbani na ushindi.

“Mashindano ya Airtel rising stars ni mashindano makubwa nandiyo maana yamepewa heshima kubwa sana na shirikisho la soka nchini TFF, hii ni nafasi ya kwenda iwakilisha Tanzania na mtakuwa mabalozi wazuri haya si mashindano ya chandimu haya ni mashindano makubwa ya dunia.”
Wambura akitafakari jambo

Akizungumza wakati wa kukabidhi bendera ya Tanzania kwa manahodha wa timu hizo mbili, katibu mkuu wa shirikisho la mpira wa miguu nchini TFF Angetile Osiah amewataka vijana kuwa wasikivu na kufata maelekezo wanayopewa na walimu wao ili kuondokana na lawama endapo timu itashindwa kufanya vizuri.

“leo mnabeba jukumu la ubalozi ni jukumu zito sana, unapokuwa balozi unatakiwa ubebe sifa zinazolingana na unachokwenda kushiriki”

“Tuna jukumu zito sana la kubeba hiyo dhamana, kwahiyo tuhakikishe kila tunachoenda kukifanya ni lazima ujiulize hiki ndicho nilichoambiwa kukifanya?”

"Nidhamu binafsi nidhamu ya ufundi na je mwalimu amekuambiaje, kufuata maelekezo ya mwalimu ni kitu muhimu sana”.
Timu ya Airtel rising stars ya wasichana ikikabidhiwa bendera ya Taifa
Timu ya Airtel rising stars ya wavulana ikikabidhiwa bendera
 
Timu zote mbele vijana 32
Utaifa mbele kila la kheri  




Hakuna maoni:

Chapisha Maoni