Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetoa
siku 14 kwa klabu za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) na za Ligi ya Daraja la Kwanza
(FDL) kuwasilisha mikataba ya makocha wao.
Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya TFF
iliyokutana Septemba 12 mwaka huu imebaini klabu nyingi hazijawasilisha
mikataba ya mabenchi yao ya ufundi, kitu ambacho ni matakwa ya kikanuni.
Siku hizo 14 zimetolewa kuanzia Septemba 17 mwaka
huu.
Kwa klabu ambazo zitashindwa kuwasilisha mikataba
hiyo na vielelezo vingine ndani ya mudau huo zitachukuliwa hatua kwa mujibu wa
kanuni.
MAKOCHA MBALIMBALI WA LIGI KUU
![]() |
Ernie Brands Yanga Afrika |
![]() |
King Kibaden Mputa Mnyamaaaaaaaaa |
![]() |
Hemed Suleiman Morocco Coastal |
![]() |
Ruvu Mkwasa mwenyeweeee Master |
Wakati huo huo mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya Simba na
Mgambo Shooting Stars iliyochezwa jana (Septemba 18 mwaka huu) katika Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam imeingiza sh. 58,365,000.
Watazamaji 10,241 walikata tiketi kushuhudia mechi
hiyo namba 23 ya VPL msimu wa 2013/2014 iliyomalizika kwa wenyeji Simba kuibuka
na ushindi wa mabao 6-0.
Viingilio katika mechi hiyo vilikuwa sh. 5,000, sh.
8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 huku kila klabu ikipata mgawo wa sh.
13,839,327.45 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh.
8,903,135.59.
Mgawo mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya
uwanja sh. 7,036,946.16, tiketi sh. 2,548,890, gharama za mechi sh.
4,222,167.70, Kamati ya Ligi sh. 4,222,167.70, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa
Miguu (FDF) sh. 2,111,083.85 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam
(DRFA) sh. 1,641,954.10.
Boniface Wambura Mgoyo
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni