Jumanne, 3 Septemba 2013

KENYA THE HARAMBEE STARS CHAENDELEA KUJIFUA



Kiungo Jamal Mohammed na mshambuliaji Dennis Oliech wanaokipigia soka nje ya Kenya, tayari wameshaungana na kikosi cha timu ya taifa ya Kenya The Harambee stars kitakachojitupa dimbani jumapili kukipiga dhidi ya Namibia katika mchezo wa mchujo wa kombe la dunia 2014.


Katika mazoezi ya jioni ya leo wachezaji 22 kati ya 27 ndiyo walioripoti wakati wengine watano wanategemewa wakati wowote kutoka sasa kujiunga na kikosi cha The Harambee.


Kocha msaidizi wa Kenya James Nandwa amesema kuwa matokeo ya mechi hiyo muhimu yatawawezesha kupata mterekemko katika michuano mingine ya FIFA pamoja na kuipandisha timu hiyo katika viwango vya ubora vya soka duniani.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni