0-0 DRAW PUTS HOLDERS AHLY AND PIRATES INTO
SEMI-FINALS
Mabingwa
watetezi wa ligi ya mabingwa barani Afrika Al Ahly pamoja na Orlando Pirates
wamefanikiwa kutinga kwenye hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo baada ya
kutoka sare ya kutofungana mjini Soweto usiku wa kuamkia leo.
Al Ahly
ktoka nchini Misri imemaliza kileleni mwa kundi A ikiwa na alama 11 na timu
hiyo itapapatuana na Coton Sport ya Cameroon kwenye nusu fainali mwezi ujao kwa
maana ya Octoba mwaka huu.
Nao
Orlando Pirates ya bondeni Afrika kusini watakwaana na Esperance ya Tunisia katika
hatua hiyo ya nusu fainali.
Hata hivyo katika mchezo huo wa hapo jana pia ulitoa
nafasi kwa wawakilishi wa Congo Ac Leopards kufuzu nusu fainali kabla ya kikosi
hicho kukubali kichapo cha mabo 4-1 toka kwa Zamalek katika mechezo uliopigwa
El Guna nchini Misri.
Leopards na Zamalek zote zimemaliza zikiwa na alama
7, alama moja nyuma ya Orlando Pirates ambao wamefanikiwa kusonga katika hatua
hiyo wakiwania kuvuka daraja la kutinga kwenye fainali ya champions league
Afrika.
TAARIFA
NYINGINE TOKEA NCHINI MISRI
Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Misri Mmarekani Bob
Brdaley ametangaza majina ya wachezaji 10 wanaokipigia nje Misri kwaajili ya
mechi zao cha mchujo hatua ya mtoano kombe la dunia 2014.
Kocha huyo anataraji kutangaza kikosi kamili hivi
karibuni atakachokitumia wakati wa mechi yao dhidi ya Ghana The Black Stars
itakayopigwa katika dimba la Baba Yara mjini Kumasi Octoba 15 pamoja na ile ya
marudiano watakayokuwa nyumbani nchini Misri mwezi mmoja baadae.
Wachezaji hao ni Mohammed Gedo, Ahmed El-Mohammed,
Hossam Ghaly, Mahmoud Kahraba na Ibrahim Salah.
Wengine ni Mohammed Salah, Mohammed El-Neny,
Al-Salmiya, Amri Zaki na Adam El-Abd.
GABON
SACK COACH PAULO DUARTE
Shirikisho
la mpira wa miguu la Gabon limemtimua kocha mkuu wa timu ya taifa ya Gabon
Paulo Duarte kufuati kikosi hicho kuondolewa kwenye kampein ya kuwania kutinga
fainali za kombe la dunia mwakani zitakazopigwa nchini Brazil.
Katika
taarifa iliyotolewa na shirikisho hilo mapema hii leo inaeleza kuwa kocha huyo
ataendelea kubaki kwenye shirikisho akiwa kama mkurugenzi wa ufundi.
Kocha huyo
aliteuliwa kukinoa kikosi cha Gabon mwezi April mwaka jana kwa mkataba wa miaka
miwili, mkataba ambao ulitaraji kumalizika mwezi April mwakani hata hivyo
tayari shirikisho limeuvunja mkataba huyo baada ya kuonekana hana msaada wowote
katika kikosi hicho.
Kocha huyo
mwenye miaka 44 mbali na kushindwa kuipeleka Gabon kwenye fainali ya kombe la
dunia mwakani pia ameshindwa kuiwezesha timu hiyo kucheza fainali za CHAN zitakozounguruma
mapema mwakani bondeni Afrika ya kusini.
SENEGAL STILL TO DECIDE ON VENUE FOR WORLD CUP
PLAY-OFF
Shirikisho la
soka la Senegal limeshindwa kutekelezwa agizo la shirikisho la soka duniani FIFA
lililowataka kukamilisha taarifa sahihi za lini na wapi watacheza mchezo wao wa
marudiano hatua ya mtoano dhidi ya Ivory Coast.
Rais wa shirikisho hilo Augustin Seghor amesema kuwa
wanataraji kukutana leo na kesho kujadili juu yaagizo hilo huku wakiwa na
pendekezo la nchi mbili ambazo ni Gine na Morocco, moja kati ya nchi hiyo
itatumika kuandaa mtanange huo.
FIFA ilitoa agizo kwa timu zote kumi ambazo
zitachuana kwenye hatua ya mtoano kupelekeza taarifa rasmi za siku husika
pamoja na viwanja vitakavyotumika kucheza mechi zao za mchujo wa kombe la dunia
ambazo za awali zinataraji kupigwa kati ya Octoba 11 hadi 15 wakati zile za
marudiano zitapigwa November 15 hadi 19 mwaka huu.
Nchi zingine ambazo pia zinakibarua kizito cha
kuwania nafasi 5 za uwakilishi wa bara la Afrika kwenye kombe la dunia mwakani
nchini Brazil ni Ivory Coast, Ethiopia, Ghana, Misri, Tunisia, Algeria,
Burkinafaso, Cameroon na Nigeria.
RWANDA:
KIGALI MTN HALF-MARATHON SET FOR OCTOBER 20
Shirikisho la riadha la Rwanda limearifu kuwa
mashindano ya riadha ya m bio fupi maarufu kama Kigali half –marathon kwa mwaka
yanataraji kufanyika Octoba 20 katika mji wa Kigali.
Mashindano hayo ya Kilometa 20 kwasasa yanadhaminiwa
na kampuni ya MTN na siyo Coca cola kama ilivyokuwa hapo awali na udhamini wa
kampuni hiyo sasa utajumuisha matangazo yote ya radio, magazeti pamoja na
television.
Katibu mkuu wa shirikisho hilo Johnson Rukundo
amesema kuwa shindano hilo litahusisha wanariadha wazawa pekee hata hivyo bado
wanajadili ni zawadi zipi zitatolewa kwa watakao ibuka na ushindi.
Ikumbukwe mshindi wa mwaka jana kwa wanaume alikuwa
ni Robert Kajuga aliyetumia muda wa dakika 57 na sekunde 12 wakati kwa wanawake
alikuwa ni Claudette Mukasakindi aliyetumia saa moja na dakika 9 na sekunde 8.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni