Jumatano, 4 Septemba 2013

MICHEZONI



WIN ENSURES QUALIFICATION FOR GHANA
Timu ya taifa ya Ghana inapewa nafasi kubwa ya kufuzu katika hatua ya mtoano ya kombe la dunia 2014 endapo wataepuka kupoteza mchezo wa o dhidi ya Zambia September 06 mwaka huu.
Ghana The Black Stars wanashikilia usukani wa kundi D wakiwa na alama 12 alama moja zaidi ya Zambia wana Chipolopolo na timu zote mbili zinalia na majeruhi waliopo vikosini hapo.
Ghana watamkosa nahodha wao Asamoah Gyan wakati kocha wa Zambia Herve Renard ameshauriwa kutafuta plan B kukiwezesha kikosi chake kuwa imara kuelekea kwenye mtanange huo.
SAINFIET RUES BOTSWANA DEFEAT
Kocha mkuu wa Malawi Tom Sainfiet amesikitishwa kuona kikosi chake kikipoteza mchezo muhimu wa kujipima nguvu usiku wa kuamkia leo ambao waliutumia kama maandalizi ya mwisho kuelekea kwenye mchezo wao wa mchujo wa kombe la dunia.
Malawi ilikubali kipigo cha goli 1-0 toka kwa Botswana ikiwa ni mchezo wa kimataifa wa kirafiki kujiandaa kuwakabili mabingwa wa kombe la mataifa Afrika Nigeria The super Eagles.
Aidha Tom amezielekeza lawama zake kwa mlinda mlango wa Malawi Charles Swini aliyeonekana kuruhusu goli la wazi lililoiharibia mipango timu yake, kitendo ambacho anakitafsiri ni uzembe wa kipa huyo.
Malawi imeondoka leo nchini Botswana kuelekea Nigeria ambako watashuka dimbani jumamosi hii kukipiga dhidi ya wenyeji wao The super Eagles wakati Malawi wakihitaji ushindi katika mchezo huo, wenyewe Nigeria sare tu inawatosha.
Wakati huo huo kikosi cha Nigeria leo kimefanya mazoezi katika uwanja wa UJ ESENE, uwanja ambao utatumika kuandaa mtanange huo.
MICHO LOOKS TO NEMESIS FOR INSPIRATION
Kocha wa kikosi cha Uganda The Cranes Milutin Sirijiovich Micho amewataka mashabiki wa soka kutokitabiria mabaya kikosi chake kuelekea kwenye mchezo wao wa kuisaka tiketi ya kutinga fainali za kombe la dunia mwakani dhidi ya Senegal.
Uganda watamenyana na Senegal wikiend hii Marakesh nchini Morocco, na hisia za mashabiki wengi wa soka barani Afrika wanauzungumzia mchezo huo utakuwa ni mwisho wa safar ya Uganda katika michuano hiyo wakati ikiwa ni tiketi kwa Senegal kufuzu katika hatua ya tatu ya mtoano.
Mchezo wa awali kati ya wawili hao uliopigwa Kampala nchini Uganda ulimalizika kwa sare ya mabao moja moja, na timu hizo zinachuana vikali wakitofautiana kwa alama moja.
NCHINI KENYA
Nahodha wa timu ya Taifa ya Kenya The Harambee stars Victor Wanyama ameungana na kikosi hicho kilichopo kambini kikijiwinda dhidi ya Namibia katika mchezo wa kukamilisha ratiba ya mchujo ya kombe la dunia mwakani nchini Brazil.
Wanyama anaungana na wachezaji wengine wa kimataifa Denis Oliech na Jamal Mohammed ambao tayari wamesharipoti mapema hapo jana.
Kocha msaidizi wa Kenya amesema kuwa kikosi chake kinaendela na mazoezi kujiimarisha kuelekea katika mchezo huo wa kundi F.
FOUR PLAYERS AT WARRIORS TRAINING
Wakati vikosi vingine vikionekana kuwa na ari kuelekea kwenye mechi zao za mchujo, huko Zimbabwe kocha mkuu wa timu taifa ya nchini humo Ian Gorowa ameshangazwa kuona kikosi hicho kikishindwa kufanya mazoezi jana na leo kutokana na asilimia kubwa ya wachezaji wake kushindwa kuripoti katika kikosi hicho.
Taarifa za ndani zinasema kuwa ni wachezaji wanne pekee ndiyo walioripoti hapo jana wakati hata viongozi wenzake wa benchi la ufundi akiwemo kocha msaidizi nao wameshindwa kujiunga na kikosi hicho kilichoingia kambini kujiandaa kuikabili Msumbiji wikiend hii.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni