TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Sisi wanachama wa timu ya PAN AFRICAN FC tunasema
hatuko tayari kufanya uchaguzi bila ya kufanyika mkutano mkuu.
Mkutano mkuu ni haki yetu kwa mujibu wa katiba Ibara
ya 20, jambo linalo sikitisha viongozi tuliowapa dhamana ya kuongoza klabu yetu
katika uchaguzi wa tarehe 18/04/2009 mpaka wanamaliza muda wao tarehe
18/04/2013 miaka mine kwa mujibu wa katiba ibara ya 29:1 hawajaitisha mkutano
mkuu hata mmoja hivyo kutunyima fursa ya kuchangia maendeleo ya timu yetu.
Mpaka hivi sasa hatujui mapato na matumizi ingawa
viongozi hao wanachukua kodi ya jingo letu,hatujui pesa hizo zinatumika kwa
matumizi gani na timu hatuna hatushiriki mashindano yoyote.
Cha kushangaza na kustaajabisha viongozi hao
wameshikilia kutaka uchaguzi na hawataki kusikia suala la mkutano mkuu na
wanaungwa mkonon na baadhi ya viongozi wa IDFA.
Sisi tunasema hatuwezi kwenda kinyume na katiba yetu
tunachowaomba viongozi wa IDFA, DRFA na TFF watuelewe sisi tunataka sana
uchaguzi lakini kwanza tufanye mkutano mkuu tujue kazi za kamati ya utendaji
kwa muda wa miaka mine waliyokaa madarakani tupatiwe mahesabu, mapato na
matumizi yaliyokaguliwa na mkaguzi anayetambuliwa kisheria kwa mujibu wa katiba
yetu, kwa kipindi chote walichokaa madarakani kinyume na hivyo hatupo tayari
kufanya uchaguzi na ikibidi tutaenda mahakamani kudai haki yetu ya kikatiba.
Hivyo wasije kutuelewa viabaya tunataka uma wapenda
soka wote watuelewe, haki tunayodai na kuitaka.
Mwisho tunatoa taarifa kwa wanachama wote wa PAN
AFRICAN FC waliolipia kadi zao na wote wasiolipia kadi zao wafike katika
mkutano utakaofanyika siku ya jumamosi tarehe 07/09/2013 shule ya msingi mnazi
mmoja saa 4:00 asubuhi kila mwanachama atakaepata taarifa hii amuarife
mwenziwe.
Taarifa imetolewa na
MZEE
ALLY ABBASY
MWANACHAMA
NO.0059
KWA
NIABA YA WANACHAMA WOTE
0755980840.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni