Kampuni ya Delina Group na Chama Cha soka cha Mkoa
wa Dar es Salaam (DRFA) kimeipiga tafu klabu cha waandishi wa habari za michezo
nchini (Taswa SC) kiasi cha sh milioni 4.2 ili kuwawezesha kushiriki katika
mashindano ya wana-habari yaliyopangwa kufanyika Jumapili ijayo mkoani Arusha.
Makabidhiano hayo yamefanyika leo kwenye mgahawa maarufu wa City Sports Lounge uliopo katikati ya jiji la Dar es Salaam. Katika makabidhiano hayo, mjumbe wa DRFA kupitia vilabu katika mkutano mkuu wa TFF, Benny Kisaka alikabidhi kiasi cha sh 1.2 huku Mkurugenzi wa kampuni ya Delina ambaye ni mdau mkubwa wa michezo nchini, Davis Mosha alikabidhi shs milioni 3 kwa mwenyekiti wa Taswa SC, Majuto “Ronaldo De Lima” Omary.
Kisaka alisema kuwa wameamua kutoa msaada huo kutokana na mchango wa waandishi wa habari za michezo nchini kwa mkoa wa Dar es salaam kwani ni wadau wao wakubwa.
Mosha alisema kuwa amesukumwa sana na mwamko wa waandishi wa habari ambao wameamua kuonyesha kwa mfano kwa kucheza soka na mpira wa pete (netiboli).
Alisema kuwa kampuni ya Delina Group imeamua kutoa mchango huo ili kuwawezesha kufanya vizuri katika mashindano hayo yaliyoandaliwa na kampuni ya Ms Unique kwa kushirikiana na Taswa Arusha na kudhaminiwa na TBL, Tanapa, Mega Trade, Pepsi, AICC na Wazee Klabu.
Mwenyekiti wa Taswa SC, Majuto Omary aliwapongeza wadau hao kwa msaada huo mkubwa. “Mbali ya DRFA na Davis Mosha, pia Azam imetupiga tafu safari hii ambapo mbali ya fedha pia wametoa jezi mbili,” alisema Majuto.
Aliwataja wadhamini wengine kuwa ni Bodi ya Ligi (TPL Board) na Kassim Dewji ambao wamechangia kufanikisha ziara hiyo. “Bado tunahitaji msaada wa hali na mali ili kuweza kufikia bajeti yetu, kwa ajili ya safari hiyo,” alisema Majuto.
Mwenyekiti wa Taswa SC, Majuto Omary akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo,juu ya mashindano yao dhidi ya Taswa FC ya jijini Arusha.
mjumbe wa DRFA kupitia vilabu katika mkutano mkuu wa TFF, Benny Kisaka akizungumza machache kabla ya kukabidhi mchango wao kwa timu hiyo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni