AfricanStar Entertainment – ASET ikishirikiana
na studio ya Fleva Inc Audio Records and
Video Production Pamoja na Makubi Sports Promotion imeandaa Tamasha
la vipaji vya Wasanii wa fani mbalimbali za sanaa kwa Wasanii ambao bado
hawajapata fursa ya kutoka na kufanikiwa kupitia sanaa zao, tamasha hilo
linatarajiwa kufanyika katikati ya mwezi Octoba ambalo litaitwa
Tamasha la Vipaji 2013.
Ndugu Waandishi , Malengo mahsusi ya Tamasha la Vipaji 2013 ni kuvionesha vipaji mbalimbali vya Wasanii ambao bado hawajapata fursa ya kuonekana pia kuhamasisha, kuendeleza na kulinda vipaji vya wasanii hao ili vipawa hivyo viwe ni sehemu ya nyenzo muhimu ya ajira za uhakika katika maisha ya vijana mbalimbali ambao wamejiingiza katika taaluma ya sanaa. Tamasha hili pia litasaidia ukuzaji wa ajira za Wasanii mbalimbali wataojitokeza.

Ndugu Waandishi, walengwa wakuu wa Tamasha la
Vipaji 2013 ni Wasanii wa Maigizo ya jukwaani (Matangazo , Filamu &
Tamthilia),Wasanii wa Vichekesho,Wasanii wa Muziki Bongofleva (R & B, Raga,
Hiphop n.k),Wasanii wa Kupiga na kucheza Ngoma za Asili,Wasanii wa kucheza
muziki wa Wasanii wa ndani au nje ya nchi,Kucheza show za nyimbo mbalimbali za
ndani na nje Kuigiza Sauti za watu mbalimbali walio maarufu wa hapa
Tanzania,Kuigiza kazi za Watangazaji maarufu wa vipindi vya Radio na
Televisheni vya Tanzania.
Wasanii wa Ubunifu wa michoroWasanii wenye vipaji
vya utangazaji wa vipindi vya radio na televisheni,pamoja na wale wa Sanaa za
maonesho ya mavazi
Ndugu Waandishi, Wasanii wataofanya vizuri katika tamasha hilo wapata fursa ya kufanya kazi (lebo) na Studio ya Fleva Inc Record, pia kushiriki katika kazi zinazoandaliwa na ASET ikiwemo filamu, tamthilia kuimba ,kucheza dance n.k. Pamoja na pia tunakaribisha kampuni /taasisi mbalimbali kusaidia kufanikisha tamasha hili pamoja na kuwasaidia Wasanii hawa kufikia malengo
Ndugu Waandishi, Fursa hii ni adimu kwa Wasanii wengi hivyo Wasanii wanaohitaji kushiriki wafike Ofisi za ASET au Fleva Inc Studio zilizopo Ukumbi wa Vijana Social Hall Kinondoni kwa ajili ya Kujiandikisha, mwisho wa kujiandikisha ni tarehe 30 Septemba 2013 saa kumi jioni,tamasha linatarajiwa kufanyika 21 Octoba 2013 katika Ukumbi wa Vijana Hall uliopo Kinondoni mjini Dar es Salaam

Nawashukuru kwa usikivu wenu tunaomba
ushirikiano.
W.R MAKUBI Project Meneja
Kwa Niaba
ASHA BARAKA
Mkurugenzi
ASET/FLEVA INC RECORDS.
Kwa Niaba
ASHA BARAKA
Mkurugenzi
ASET/FLEVA INC RECORDS.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni