Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika
(CAF) limemteua Leslie Liunda wa Tanzania kuwa mtathmini wa waamuzi kwenye
mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Coton Sport ya Cameroon na Esperance
ya Tunisia.
Mechi hiyo ya kundi B itachezwa
Septemba 21 mwaka huu kwenye Uwanja wa Omnisport Roumdeadjia mjini Garoua,
Cameroon. Kamishna atakuwa Bema Doumbia wa Ivory Coast.
Waamuzi wanatoka Madagascar
wakiongozwa na Hamada Nampiandraza. Wasaidizi wake ni Jean Eric Pierre
Andrivoavonjy, Ferdinand Velomanana Linoro na Bruno Marie Andrimiharisia.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni