Ligi kuu nchini Kenya KPL itasimama kwa muda wikiend
hii kupisha mchezo wa kimataifa kati ya wenyeji Kenya The Harambee stars dhidi
ya Namibia.
Kenya itashuka dimbani jumapili hii September 08
kuikabili Namibia, katika mchezo wa kuwania nafasi ya kutinga kwenye fainali za
kombe la dunia mwakani nchini Brazil.
Shirikisho la mpira wa miguu la Kenya limesema kuwa
mwishoni mwa wiki hii watakuwa na kibarua kizito kuisaidia timu yao kuibuka
kidedea katika mchezo huo, ndiyo maana wamelazimika kusimamisha mechi zote za
ligi zilizopaswa kupigwa kuanzia ijumaa hadi jumapili.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni