JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MALIASILI NA UTALII
TAARIFA KWA UMMA
Katibu Mkuu wa Wizara
ya Maliasili na Utalii Bi. M.K.Tarishi amemteua Bw. Chikambi Karugendo Rumisha (57) kuwa Kaimu Mkuu
wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali na Msemaji wa Wizara ya Maliasili na
Utalii.
Katibu Mkuu amefanya
uteuzi huo kwa mamlaka aliyo nayo chini ya Kifungu cha 6 (b) cha Sheria ya
Utumishi wa Umma Na. 2003.
Bw. Rumisha ameitumikiwa
Wizara tangu mwaka 1984 katika idara mbalimbali hali inayompa uzoefu na uelewa
mkubwa wa masuala mbalimbali yanayohusu Wizara ya Maliasili na Utalii.
Kabla ya uteuzi huo Bw. Rumisha alikuwa akitumikia Wizara ya Maliasili
na Utalii katika Idara ya Sera na Mipango.
Bw. Chikambi Rumisha ambaye ni mtaalam wa elimu
viumbe alihitimu Shahada ya Sayansi – Ekolojia ya Bahari na Wanyama katika Chuo
Kikuu cha Dar es Salaam mwaka 1984.
Ahitimu masomo ya Uzamili katika fani ya
Uvuvi na Viumbe wa Bahari Mwaka 1987 katika Chuo Kikuu cha Bergen, Norway. Amehudhuria Mafunzo mbalimbali ya muda
mfupi ndani na nje ya nchi katika masuala ya mipango, utawala, fedha;
ufuatiliaji na upelembaji, Mawailiano, na usimamizi wa miradi.
Bw. Rumisha ameitumikia Serikali katika vituo
mbalimbali, pamoja na Makao Makuu ya Wizara idara ya Uvuvi alipohudumu kama
Afisa Uvuvi, Kilichokuwa Chuo cha Uvuvi Nyegezi- Mwanza alipohudumu kama
mkufunzi, Marine Parks alipohudumu Kama Meneja na Mwazilishi wa Taasisi hiyo
na Makao Makuu ya Wizara -Idara ya Sera na Mipango kitengo cha
Ufuatiliaji
Uteuzi huu wa Bw. C.K.Rumisha unafuatia
kustafu kwa aliyekuwa Mkuu wa Kitengo cha Mawasilino ya Serikali wa Wizara, Bw.
George Matiko kustaafu tangu tarehe 15/06/2013.
Bw. Chikambi K Rumisha uteuzi wake
unanzia tarehe 15/8/2013 na utadumu hadi hapo itakapoamuliwa vinginevyo.
Katibu Mkuu
Wizara ya Maliasili na Utalii
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni