Ijumaa, 6 Septemba 2013

JUMA K JUMA BADO CHAGUO LA KIM PAULSEN




KOCHA Mkuu wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Mdenmark Kim Poulsen anatarajiwa kuendelea kumuanzisha kipa Juma Kaseja katika mchezo wa kesho dhidi ya Gambia mjini hapa kukamilisha ratiba ya mechi za kufuzu Kombe la Dunia mwakani Brazil.

Nahodha wa Stars, Kaseja hana timu kwa sasa baada ya kutemwa Simba SC, lakini mbele kocha Kim ameendelea kuwa lulu.

Kwa ujumla, katika mchezo wa kesho, kikosi cha kinatarajiwa kupangwa hivi; Juma Kaseja, Vincent Barnabas, Erasto Nyoni, Nadir Haroub, Henry Joseph, Frank Domayo, Haruni Chanongo, Amri Kiemba, Mrisho Ngasa, Simon Msuva na Khamis Mcha


Mechi hiyo itaanza saa 10.30 jioni kwa saa za hapa ambapo nyumbani Tanzania itakuwa saa 1.30 usiku, na itachezeshwa na waamuzi kutoka Rwanda Munyemana Hudu. Waamuzi wasaidizi ni Theogene Ndagijimana, Honore Simba na Issa Kagabo. Kamishna ni Andy Quamie kutoka Liberia.

Washabiki na vyombo vya habari vya hapa wanaizungumzia mechi hiyo ambayo ina umuhimu mkubwa kwa pande zote, huku Gambia ikiwa imeita wachezaji tisa wanaocheza barani Ulaya na Marekani.
Gambia ambayo imepata uongozi mpya wa Chama chake cha Soka (GFA) imepania kuhakikisha haimalizi mechi za mchujo ikiwa na pointi moja tu.

Kocha Poulsen amesema nia ni kuona Stars yenye pointi sita inamaliza katika nafasi ya pili nyuma ya Ivory Coast ambayo tayari imechukua tiketi pekee ya kucheza raundi ya mwisho kutoka kundi hili la C.
 “Mechi hii ni muhimu kwetu kwa vile tunataka matokeo mazuri ugenini. Lakini kikubwa ni kuwa matokeo mazuri si tu yatatuweka katika nafasi ya kuwa wa pili, lakini vilevile yatatusaidia kuongeza pointi kwenye viwango vya ubora vya FIFA, na kikubwa zaidi hii ni sehemu ya maandalizi ya sisi kucheza Fainali za Afrika za 2015,” amesema Kim.

Kikosi cha Taifa Stars kimewasili salama hapa Banjul, Gambia tayari kwa mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia dhidi ya wenyeji itakayochezwa kesho (Septemba 7 mwaka huu

stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager imewasili hapa jana (Septemba 5 mwaka huu) saa 11 jioni ikitokea Dakar, Senegal ambako ilichelewa kuunganisha ndege, hivyo kuamua kutumia usafiri wa barabara kwa vile ni karibu na baadaye kupanda kivuko kuingia Banjul badala ya kulala na kuchukua ndege nyingine siku inayofuata.

Wachezaji wako katika hali nzuri na leo jioni wanatarajia kufanya mazoezi ya mwisho kwenye Uwanja wa Independence ulioko Bakau ambao utatumika kwa mechi ya kesho. Timu imefikia hoteli ya Sea View Garden iliyopo kandokando ya Bahari ya Atlantic

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni