Jumatano, 4 Septemba 2013

TUME YA USHINDANI YAKAMATA BIDHAA BANDIA ZENYE THAMANI YA SH.MIL 44.2/-





Mabingwa wa zamani wa ligi kuu wekundu wa msimbazi Simba wametoa siku 6 kuanzia hii leo hadi September 09 mwaka huu kwa yoyote anaehusika na kuuza bidhaa feki za Simba kujisalimisha klabuni hapo ikiwa ni utekelezaji wa oparesheni mpya ya kamatakamata bidhaa feki zenye nembo ya Simba Tanzania nzima.


Mwenyekiti wa wadhamini wa Simba Mzee Hamis Kilomoni amebainisha kuwa oparesheni hii ni non-stop na mpaka sasa cwamefanikiwa kukamata bidhaa zinazoshukiwa kuwa bandia zenye thamani ya zaidi Shilling Million 44,195,000/=./



Kutoka jeshi la polisi, Inspector Mohammed mwenye dhamana ya kuwakamata watakaobainika kujihusisha na vitendo hivyo ameahidi kulivanjia njuga hilo pamoja na kuwatia kwenye mikono ya sheria kwawote watakothibitika kuhusika kwa namna moja ama nyingine.


Nae afisa mwandamizi, mawasiliano na mahusiano ya umma kutoka tume ya ushindani Frank Mdimi ambao wanahusika na uendeshaji wa oparesheni hiyo ya kushitukiza katika sehemu mbalimbali, akamtilia msisizito namna wanavyopaswa kujisalimisha ili kuokoa mapato ya klabu husika.

 SEHEMU YA BIDHAA ZILIZO KAMATWA


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni