Siku moja baada ya kutimuliwa kwenye benchi la ufundi
la AFC Leopards, mbelgiji Luc Emayl ameibuka na kutupa kijembe kwenye uongozi
wa klabu hiyo kuwa tayari ameshapata dau nono zaidi katika klabu moja
inayofanya vizuri barani Afrika.
Hapo jana Kamati tendaji ya AFC Leopards ilimtimua
Mbelgiji huyo aliyekuwa akikinoa kikosi hicho pamoja na wasaidizi wake wa
benchi la ufundi kwa kile kinachodaiwa walishindwa kuipa matokeo mazuri timu
hiyo.
Pamoja na mambo mengine kocha huyo amesema hana
kinyongo kwa maamuzi yaliyofikiwa kwakuwa tayari ameshapata timu mbadala ambayo
pia amesita kuiweka hadharani ni timu gani.
Katika hatua nyingine kocha mpya wa AFC Leopards
James Nandwa tayari ameanza kibarua chake rasmi hii leo, huku akiahidi
kuisaidia timu hiyo kwa hali na mali kuhakikisha kinafanya vizuri kufikia
malengo yake iliyojiwekea.
Nandwa ambaye pia ni kocha msaidizi wa timu ya taifa
ya Kenya The Harambee stars alitangazwa hapo jana kubeba mikoba ya mbelgiji huyo
akisaidiwa na Mickey Weche kuelekea mwishoni mwa msimu huu wa ligi.
WAKATI
HUO HUO
Timu ya taifa ya wanawake ya mpira wa kikapu nchini
Kenya imeondoka leo kuelekea Maputo nchini Msumbiji kwaajili ya kushiriki
michuano ya ubingwa wa mpira wa kikabu inayotaraji kuunguruma kuanzia September
20 hadi September 29 mwaka huu.
Kenya wamepangwa kwenye kundi B wakiwa sambamba na
timu kutoka Angola, Mali, Cameroon, Cape Verde na Nigeria wakati kundi A
linajumuisha timu kutoka Senegal, Ivory Coast, Misri, Zimbabwe na wenyeji
Msumbiji.
Kenya itaanza kampeni yake ijumaa hii dhidi ya
Cameroon wakati mmoja wa wachezaji wanaounda kikosi hicho Samba Mjomba amesema
kuwa kikosi chake kipo tayari kimejiandaa vya kutosha wanachohitaji ni kujitupa
kwa biii ili kurejea nyumbani na ushindi.
ETO’O WILL BE INVITED FOR KNOCKOUTS
Kocha msaidizi wa timu ya taifa ya Cameroon Martin
Ndtoungou amesisitiza kuwa mshambuliaji mpya wa Chelsea Samuel Etoo ataendelea
kubaki kuwa nahodha na chaguo la kwanza la kikosi hicho.
Etoo alitangaza kustaafu kuitumikia timu yake ya
taifa saa chache baada ya kumalizika kwa mchezo wao dhidi ya Libya juma
lililopita.
Kocha huyo amesema kuwabado wanamtambua kuwa Etoo ni
nahodha wa timu yao kwakuwa hajavunja mkataba wa kuitumikia timu yake ya taifa
wala kutuma taarifa rasmi ya kustaafu hivyo hivyo kauli yake itabaki kuwa kauli
aliyoitamka mbele ya wachezaji wenzake na wala siyo taarifa kwa shirikisho.
Tayari Cameroon imeonesha nia ya kumuita
mshambuliaji huyo wakati wa mechi zake za mtoano mchujo wa kombe la dunia dhidi
ya Tunisia mwezi Octoba na mwezi Novemba mwaka huu.
HUKO TUNISIA
nahodha wa zamani wa Uholanzi Ruud Krol amekubali kuingia mkataba wa miezi
miwili kuinoa kikosi cha timu ya taifa ya Tunisia kuelekea kwenye mechi zake
mbili za mchujo wa kombe la dunia 2014.
Taarifa za kocha huyo
kusaini mkataba hii leo, zimebainika kupitia mtandao wa shirikisho la mpira wa
miguu la Tunisia.
Kocha huyo sasa rasmi kuanza
kazi akirithi mikoba ya Nabil Maaloul aliyeamua kujiweka kando na timu hiyo
kufuatia kichapo cha magoli 2-0 walichopokea toka kwa Cape Verde katika mchezo
wa mwisho wa makundi September 7 mwaka huu.
Ikumbukwe Tunisia imetinga kwenye hatua hiyo ya
mwisho ya mchujo kutokana na Baraka za shirikisho la mpira wa miguu duniani
FIFA ambalo liliwazawadia timu hiyo alama tatu baada ya kujiridhisha kuwa Cape
Verde ilimtumia mchezaji asiye na sifa wakati wa mechi yao hiyo.
FIFA WANTS PLAYOFF DATES BY FRIDAY
Shirikisho la mpira wa miguu duniani FIFA
limesisitizia timu zote kumi ambazo zimetingwa kwenye hatua ya mwisho ya mchujo
wa kombe la dunia, kuthibitisha tarehe na eneo husika wakatayocheza mechi zao
husika hadi kufikia ijumaa ya September 20 mwaka huu.
Timu hizo ni Ivory Coast, Senegal, Ethiopia,
Nigeria, Ghana, Misri, Tunisia, Algeria, Burkina Faso na Cameroon.
Mechi za mkondo wa kwanza ambazo zitapigwa nyumbani
zimepangwa kati ya Octoba 11 hadi 15 wakati zile za marudiano zimepangwa kati
ya Novemba 15 hadi 19 mwaka huu.
Kwa mujibu wa ratiba Ivory coast wataanzia nyumbani
dhidi ya Senegal, Ethiopia wakiialika Nigeria, huku Tunisia ikipapatuana na
Cameroon.
Mechi zingine Algeria watakuwa wenyeji wa Burkina
Faso wakati Ghana watamenyana na Misri.
Hata hivyo tayari Ghana wameshatuma majibu kwa FIFA
wakilichagua dimba la Baba Yara lililopo Kumasi pamoja na kuichagua Octoba 13
kuwa ni siku itakayotumika kucheka mchezo huo wa awalia.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni