GHANA REACH LAST PHASE OF QUALIFIERS
Timu ya
Taifa ya Ghana imefanikiwa kutinga kwenye hatua ya tatu ya mtoano ya kombe la
dunia baada ya jana kumtandika Zambia magoli 2-1 katika mchezo wa mchujo wa kundi D.
Ghana The
Black Stars sasa inaungana na Algeria, Misri na Ivory katika hatua hiyo ya tatu
ya mtoano ambapo washindi wa jumla wa makundi yote kumi watachuana katika mechi
za nyumbani na ugenini ili kuwapata wawakilishi wa bara la Afrika katika
michuano ya kombe la dunia itakayounguruma mwakani nchini Brazil.
Ghana
ilikuwa ni nchi pekee ya Afrika iliyong’ara kwenye michuano ya kombe la dunia
iliyopita, baada ya kufanikiwa kutinga hadi kwenye robo fainali ikiondolewa
kishujaa kwa mikwaju ya penalty dhidi ya Uruguay.
DIPELA EXPLAINS CHAN DRAW DECISION
Mwenyekiti
wa michuano ya mataifa bingwa barani Afrika CHAN Andrew Dipela ameelezea uamuzi
wa kuliteua jiji la Cairo nchini Misri kutumika katika zoezi la upangaji wa
ratiba ya CHAN na si Afrika kusini kama wengi walivyodhani hapo awali.
Ikumbukwe
Afrika kusini ndiyo wenyeji wa michuano hiyo ambapo itashudiwa timu 16
zikichuana kuwania ubingwa huo pamoja na mambo mengine bado haijawa kigezo cha
kamati ya mashindano kuipa heshima ya upangaji wa ratiba nchini hiyo ambayo
itafanyika September 18 mwaka huu.
Inasemekana
siku mbili kabla ya upangaji wa ratiba hiyo, pia katika jiji hilo kutakuwa na
upangaji wa ratiba ya mechi za mtoano za mchujo wa kombe la dunia 2014.
Timu zote
16 zilizofanikiwa kutonga kwenye fainali za CHAN zinataraji mapema mwezi ujao
kupigwa msasa kuelekea kwenye michuano hiyo itakayounguruma mwezi January mwakani.
KARUTURI SUSPEND COACH OMONDI
Siku moja
baada ya uongozi wa Karuturi sport kumsimamisha kocha mkuu wake James Omondi,
kocha huyo umeibuka na kudai hana kinyongo na maamuzi hayo licha ya kushangazwa
na hatua hiyo.
Katika
barua iliyotumwa kwa shirikisho la soka la Kenya Alhamis ya wiki hii, Uongozi
wa Karuturi umetanabahisha kuwa umemsimamisha kocha huyo kutokana na kushindwa
kuipa matokeo mazuri timu yao inayoshiriki ligi kuu nchini humo.
James
Omondi ambaye ni kocha msaidizi wa zamani wa Thika United alijiunga na kikosi
cha Karuturi mapema mwaka huu akirithi mikoba ya Michael Nam aliyeamua kuachana
na kibarua hicho ili kujiendeleza kitaaluma.
Toka
ajiunge na klabu hiyo ambayo kwasasa inakamata mkia wa ligi nchini Kenya,
Omondi ameiweza kushinda michezo miwili, kudraw michezo sita na kufungwa
michezo nane, hatua ambayo imewawezesha kutwaa alama 16 pekee, zikiwa ni alama
25 nyuma ya vinara wa ligi hiyo Gor Mahia.
STADIUM DILEMMA CONTINUES FOR EGYPT
Shirikisho
la mpira wa miguu la Misri bado liko njia panda likihaha kutafuta kiwanja
kitakachotumika kuandaa mchezo wa mchujo wa kombe la dunia kati ya timu ya
Taifa ya Misri dhidi ya Gine jumanne ijayo.
Awali
shirikisho hilo lilitangaza dimba la Borg Al Arab kuwa mwenyeji wa mtanange huo
kabla ya wizara ya mambo ya ndani ya Misri kuzuia kiwanja hicho kuumika
kutokana na sababu za kiusalama.
Kocha
msaidizi wa Misri Diaa Al Sayed amesema kuwa mpaka sasa bado hawajajuwa ni wapi
watacheza mchezo huo, wanasubiri taarifa ya shirikisho la soka nchini humo
ambalo limeahidi kutavunja kiwanja mbadala kabla ya kufikia September 10 mwaka
huu.
Misri
ndiyo vinara wa kundi G wakiongoza kwa alama 15 na tayari imeshafuzu kwenye
hatua ya tatu ya mtoano itakayoanza kupigwa mapema mwezi November.
Misri
watakuwa wenyeji wa Gine September 10 mwaka huu wakati Algeria ikiwaalika Mali
katika mchezo wa kundi H.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni