Jumatano, 4 Septemba 2013

BARAZA LA WAZEE YANGA LAMFURUMUSHA PARTIC NAGGI AMBAYE ANADAIWA KUWA KATIBU MPYA WA YANGA



Siku moja baada ya mabingwa wa ligi kuu Yanga Afrika kudaiwa kupata katibu mpya, baraza la wazee la Yanga limekanusha kumtambua katibu huyo na kumtaka aondoke mara moja klabuni hapo.


Katibu huyo mpya Patric Naggi raia wa Kenya inadaiwa ameletwa kukalia kiti cha kaimu katibu mkuu wa sasa Lawrence Mwalusako bila ya kutokuwepo taarifa rasmi kutoka katika kamati tendaji ya Yanga chini ya Mwenyekiti wake Yusuph Mehboob Manji.


Katibu wa baraza hilo la wazee laYanga Ibrahim Omary Akilimali “Abramohvich” amesema kuwa ujio wa Patric Naggi umekuwa ni wa mashaka kwasababu si mwanachama wa Yanga na hastahili kushika wadhifa wowote klabuni hapo kwamujibu wa katiba ya Yanga.


Mzee Akilimali ametaja kuwa ujio wa Patrick Naggi, kamati tendaji haina taarifa, baraza la wazee hawana taarifa, baraza la wenyeviti na makatibu wa mikoa pia hawana taarifa na kamati tendaji ilipaswa ipitishe taarifa ya ujio wa katibu huyo mpya.



Baraza likaenda mbali zaidi na kusema kuwa hawamtambui katibu huyo na si mwanachama wa yanga hivyo hawataki alete mgawanyiko miongoni mwa wanachama kwa kuwa ujio wake hauna utofauti na tapeli.

Sababu kubwa za baraza hilo kutoutambua ujio wake ni kutokana na kutokuwepo taarifa rasmi lakini pia inaelezwa kuwa hakuwa na mwenyeji wowote.  “tunawasiwasi asije kuwa ni tapeli hivyo hatumtambui, arudi kwa walomleta kama wapo wampe pesa ya kulala na chakula pamoja na tiketi leo arudi kwao Kenya”

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni