Pambano la Ligi Kuu ya Vodacom (VPL)
kati ya wenyeji Azam na Yanga lililochezwa jana (Septemba 22 mwaka huu) katika
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam imeingiza sh. 138,188,000.
Watazamaji waliokata tiketi
kushuhudia pambano hilo namba 33 la VPL msimu wa 2013/2014 lililomalizika kwa
Azam kuibuka na ushindi wa mabao 3-2 walikuwa 24,020.
Viingilio katika mechi hiyo vilikuwa
sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 huku kila klabu ikipata mgawo wa
sh. 33,065,409.1 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh.
21,079,525.42.
Mgawo mwingine wa mapato hayo ni asilimia
15 ya uwanja sh. 16,812,919.89, tiketi sh. 5,022,342, gharama za mechi sh.
10,087,751.93, Kamati ya Ligi sh. 10,087,751.93, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa
Miguu (FDF) sh. 5,043,875.97 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam
(DRFA) sh. 3,923,014.64.
Mechi iliyopita ya VPL kwenye uwanja
huo kati ya Simba na Mbeya City iliingiza sh. 123,971,000.
WAKATI HUO HUO Mechi namba 12 ya Ligi
Daraja la Kwanza (FDL) kati ya Toto Africans na Polisi Dodoma iliyokuwa ichezwe
Jumamosi (Septemba 28 mwaka huu) Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza imesogezwa
mbele kwa siku moja.
Timu
hizo za kundi C sasa zitapambana Jumapili (Septemba 29 mwaka huu) kwenye uwanja
huo huo ili kupisha mechi namba 10 kati ya Pamba na Stand United FC ya
Shinyanga itakayochezwa Jumamosi (Septemba 28 mwaka huu).
Mechi
nyingine za kundi hilo zitakazochezwa Jumamosi ni Mwadui na Polisi Tabora
(Uwanja wa Kambarage, Shinyanga) wakati Kanembwa JKT na Polisi Mara zitacheza
kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma.
Boniface
Wambura Mgoyo
Ofisa
Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni