Timu ya Taifa ya
Tanzania Taifa stars imeendelea na maandalizi kujiandaa kuelekea kwenye mchezo
wao dhidi ya Gambia september 08 mwaka huu nchini Gambia ikiwa ni mchezo wa
kukamilisha ratiba ya mchujo ya michuano ya kombe la dunia 2014
Aidha imeelezwa kuwa ligi kuu imepelekea kikosi cha Stars kukosa mchezo mmoja wa kimataifa kirafiki kujiandaa kuelekea kwenye mchezo wao wa September 08 mwaka huu dhidi ya Gambia
Taifa stars
inakamata nafasi ya tatu kundi CHE ikiwa na alama 6 ikizidiwa alama 7 na vinara
Ivory Coast
Morocco wenyewe
wako katika nafasi ya pili wakiwa na alama 8 wakati Gambia wakifunga dimba kwa
alama yao 1
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni