Kiungo wa kimataifa wa timu ya Taifa ya Rwanda
Haruna Niyonzima ambaye pia ni mchezaji wa mabingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom wa
timu ya Young Africans amepatwa na janga la kuunguliwa kwa baadhi ya mali zake
kufuatia kutokea shoti ya umeme leo asubuhi.
Niyonzima ambaye anaishi eneo la Magomeni Makuti
amekutwa na na tatizo hilo leo asubuhi majira ya saa 12 akiwa anajiandaa
kuelekea mazoezini ndipo alipoona moshi ukifuka kutokea eneo la sebuleni kwake
na aliposogea alibani ni moto ulikuwa ukiwaka.
"Nilisikia hewa nzito ndani, nikaamka kuelekea
sebuleni, nilipofika nilikuta moto umetanda chumba kizima ndipo majirani
walijitokeza na kuanza kutusaidia kuzima moto huo kwa kuvunja madirisha ya vioo
na kumwaga maji ili moto huo uzime" alisema Niyonzima
Nashukuru tulifanikiwa kuuzima moto baada ya muda
kwa kushirikiana na majirani lakini vitu vyote vilivyokuwa ndani hatukufanikiwa
kuivitoa vikiwa salama, baadhi ya vitu vilivyoungua ni pamoja na Luninga
iliyokua imefungwa ukutani, redio (music system), makochi na fenicha za ndani.
Aidha Niyonzima amesema moto huo utakua umetokana na
shoti ya umeme juu ya dali kwani ndio sehemu inayooenekana kuwa chanzo cha
moto.
Afisa Habari wa klabu ya Yanga SC Baraka Kizuguto
alifika nyumbani kwa Niyonzima majira ya saa 2 kasorobo asubuhi kuongea na
mchezaji ambaye alisema anashukuru familia yake wote wako salama na hakuna
aliyedhurika zaidi ya vitu vilivyoteketea na moto.
Uongozi wa klabu ya Yanga SC unampa pole Niyonzima
kwa matatizo yaliyomfika, Mungu amjalie nguvu na uvumilivu na kusema upo nae
pamoja katika wakati huu mgumu.
TAZAMA PICHA KATIKA MATOKEO TOFAUTI (kwa hisani ya Salehjembe.blogspot.com na Youngafricans.cotz)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni