Jumanne, 8 Oktoba 2013

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

REDD’S ORIGINAL YAZINDUA TAMASHA LA MITINDO KWA VYUO VYA ELIMU YA JUU (REDD’S UNI – FASHION BASH 2013)

Dar es Salaam,08 OCTOBER 2013:

Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia kinywaji chake cha Redd’s Original leo imezindua tamasha la aina yake la mitindo kwa vyuo vya elimu ya juu. Tamasha hili litakalojulikana kama “Redd’s Uni-Fashion Bash” kwa mwaka huu litaanza mwezi huu wa Octoba hadi Novemba na kushirikisha vyuo vyote vya elimu ya juu vilivyo katika mikoa minne ambayo ni Dar Es Salaam, Kilimanjaro, Iringa na Mwanza.
Kutoka kulia Meneja masoko TBL Fimbo Butallah, kushoto Meneja wa habari na mawasiliano wa TBL Edith Mushi
Akizungumza katika uzinduzi huo, meneja Masoko wa Tbl Fimbo Buttalah alisema; “Tamasha hili la mitindo lina lengo la kuinua vipaji vya wanafunzi wa vyuo katika tasnia ya mitindo kupitia maonesho yatakayofanywa katika vyuo, ambapo wanafunzi wenye vipaji vya ubunifu watapata fursa ya kuonesha ubunifu wao wa mitindo. Hii ni fursa kubwa kwao kujitangaza na kudhihirisha uwezo wao.”
 Bwana Fimbo, pia alielezea utaratibu wote wa kuwapata wabunifu watakaoonesha kazi zao jukwaani wakati wa matamasha haya ya aina yake kwa kusema; “Uzinduzi huu utafuatiwa na usajili wa wanafunzi wabunifu na wanamitindo kupitia fomu maalum zitakazosambazwa vyuoni, kisha majaji watachambua fomu zote zilizowasilishwa na kupata wabunifu 10 katika kila mkoa watakaokidhi vigezo, ambao watapata fursa ya kuonesha mavazi yao siku ya tamasha, pia kutakuwa na nafasi 10 kwa wanamitindo watakaovaa mavazi hayo jukwaani. Majaji wataangalia vigezo na kupata washindi ambao watapata zawadi toka kwa kinywaji cha Redd’s Original.”

Akizungumzia zawadi kwa washindi, meneja mawasiliano na Habari wa Tbl Edith Mushi alisema; Zaidi ya kuwapatia jukwaa wabunifu na wanamitindo hawa ili waweze kuonesha vipaji vyao, Redd’s pia itawapatia zawadi za pesa washindi watano katika kila mkoa watakaoshika nafasi za juu kama ifuatavyo;
WABUNIFU


MSHINDI WA KWANZA
700,000


MSHINDI WA PILI
500,000


MSHINDI WA TATU
300,000


MSHINDI WA NNE NA WA TANO
100,000
KILA MMOJA




WANAMITINDO


MSHINDI WA KWANZA
500,000


MSHINDI WA PILI
400,000


MSHINDI WA TATU
300,000


MSHINDI WA NNE NA WA TANO
100,000
KILA MMOJA

Tuna imani kubwa kuwa zawadi hizi zitaongeza chachu kwa wabunifu kujidhatiti katika kuendeleza ubunifu katika tasnia hii ya mitindo. Lakini pia matamasha haya yatahusisha burudani mbalimbali za kuvutia na hivyo kuwa sehemu muhimu ya kuwakutanisha wanafunzi wa vyuo na kada mbalimbali katika kufurahia na kubadilishana mawazo juu ya masuala ya ubunifu na mitindo.
Kinywaji cha Redd’s Original kimekuwa mstari wa mbele katika kuendeleza tasnia ya urembo, ubunifu na mitindo hapa nchini.


Kuhusu TBL
Tanzania Breweries Limited (TBL) inatengeneza, kuuza na kusambaza bia, vinywaji vyenye ladha ya matunda vilivyo na kilevi na vinywaji visivyo na kilevi hapa Tanzania. TBL pia ndiyo kampuni mama ya Tanzania Distilleries Limited pamoja na kampuni shiriki ya Mountainside Farms Limited.

Bia zinazotengenezwa na kampuni ya TBL ni pamoja na Safari Lager, Kilimanjaro Premium Lager, Ndovu Special Malt, Castle Lager, Vinywaji vingine vinavyotengenezwa na kundi la makampuni ya TBL ni Konyagi Gin, Amarula Cream, Redd’s Original na Grand Malt.

Kundi la makampuni ya TBL limeorodheshwa kwenye Soko la Hisa la Dar es Salaam, limeajiri watu wapatao 1,300 na linawakilishwa nchi nzima na viwanda vinne vya bia, kiwanda kimoja cha kutoneshea, kimoja cha kutengenezea kimea pamoja na bohari nane za kusambazia bia.


Kuhusu SABMiller
SABMiller plc moja kati ya makampuni makubwa ya bia duniani ikiwa na mikataba ya kutengeneza na kusambaza bia kwenye nchi zaidi ya 60 katika mabara matano. Bia zake ni pamoja na zile za kimataifa kama Miller Genuine Draft, Peroni Nastro Azzurro na Pilsner Urquell vilevile na bia nyingine zinazoongoza kwenye masoko ya ndani ya nchi mbalimbali. Nje ya Marekani, SABMiller ni moja ya kati ya makampuni makubwa yanayotengeneza vinywaji vya Coca-Cola duniani. Hivi karibuni SABMiller plc ilinunua kampuni ya bia ya Foster’s pamoja na shughuli zake za uzalishaji nchini India.
SABMiller imeorodheshwa kwenye masoko ya hisa ya London na Johannesburg.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni