![]() |
Toka huna chako hapa ole wako urudi |
Mabingwa wa zamani wa ligi kuu wekundu wa msimbazi
Simba hawatarajii kumrejesha kikosini aliyekuwa mlinda mlango wao namba moja
Juma K Juma(Juma Kaseja) walitemana nae
mwishoni mwa msimu uliopita.
Mwenyekiti wa wekundu hao Ismail Aden Rage amesema
kuwa suala la Kaseja litabaki kuwa historian a wala hawafikirii kumrejesha tena
kipa huyo kwakuwa tayari wanae kipa chaguo lao Mganda Abel Dhaira.
Rage amesema kuwa maneno yanayozungumzwa na
kuandikwa kwenye baadhi ya vyombo vya habari kuwa Kaseja atarudi Simba ni ya
uchochezi na yana lenga kuwavuruga tu.
![]() |
Dah jamani hamnionei hata huruma? |
“Hii habari ya Kaseja karudi Simba inawasaidia nini
wanasimba?tuko kwenye premier League ni kutaka kuwavuruga wanasimba waache
kuconcentrate kwenye mambo yao, dirisha dogo bado, usajili bado aliyekwambieni
tunabadilisha golikipa nani.”
![]() |
Hakatiw mtu hapa |
Tuandike vitu ambavyo vinatusaidia kuleta maendeleo,
kila siku mnaandika habari za uwongo yanga kafanya hivi simba kafanya hivi”.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni