Kocha mkuu wa mabingwa watetezi wa ligi kuu soka ya
Tanzania bara Yanga Afrika Ernie Brands amewatuliza mashabiki wa Yanga na
kuwataka kuacha kuwashutumu baadhi ya wachezaji kuwa wanatumiwa kwa namna moja
ama nyingine kuihujumu timu hiyo.
Kauli ya Brands imekuja baada ya kusikitishwa na kauli za baadhi ya mashabiki
wa Yanga waliojitokeza jana uwanja wa Taifa Dar es Salaam wakati wa mchezo wao
uliomalizika kwa Yanga kuondoka na alama 3 baada ya kuwabanjua Mgambo JKT
magoli 3-0.
Baadhi ya mashabiki wa Yanga walionekana kuendelea
kumlaumu mlinda mlango namba moja wa Yanga Ally Mustapha Mtinge Barthez pamoja
na nahodha wao Nadir Haroub Ally Canavaro kwa kile wanachokidai walipokea mpunga
na kusababisha kutoka sare na watani wao wa jadi wekundu wa msimbazi Simba.
Brands amesema kuwa hayo yote ni matokeo ya mchezo
na wala mashabiki hawapaswi kumlaumu mtu yoyote na badala yake waunge mkono
juhudi zinazofanywa na wachezaji wao za kuhakikisha wanatetea ubingwa msimu huu
wa ligi.
“They have to support us
and not blaming goalkeeper, if someone made a mistake they have to help us and
support us in good times and bad times”
Nae Dakatari mkuu wa Yanga Afrika Nassor Ally
Matuzya akafunguka kuhusiana na majeruhi waliopo kikosini hapo na endapo
kutakuwa na uwezekano wa kuwa na kikosi chote kamili kuelekea katika mchezo huo
dhidi ya JKT Ruvu.
“Kikosi kinaendelea vizuri, tuna majeruhi wachache
akiwemo Nizar Khalfani ana majeruhi ya paja kwa nyuma, yupo David Luhende
ambaye pia nae anasumbuliwa na paja, Nizar aliumia mazoezini wakati Luhende
aliumia wakati wa mechi iliyopita dhidi ya Rhino Rangers”.
“Tunae pia majeruhi Juma Abdul ambaye aliumia mechi
iliyopita pamoja na Abdallah Mghui Messi timu inaendelea vizuri na wengine wote
wanaendelea na maandalizi”.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni