Alhamisi, 31 Oktoba 2013

HAKUNA ZAIDI YA MIAKA 17 HAPA




Shirikisho la mpira wa miguu la Nigeria limesisitiza kuwa hakuna mchezaji yoyote kati ya wachezaji 21 wanaoiwakilisha nchi hiyo kwenye michuano ya kombe la dunia kwa vijana chini ya miaka 17 aliyevuka umri huo.
Msisitizo wa shirikisho hilo umekuja siku moja baada ya kutuhumiwa kuwa wamechanganya kikosi hicho na wachezaji waliovuka miaka 17 na ndiyo maana wamekuwa wakipata ushindi mnono tofauti na timu zingine.
Kikosi cha Nigeria kiliibanjua Iran magoli 4-1 katika raundi ya 16 ya michuano hiyo matokeo ambayo yamezua maneno kuwa kikosi hicho kimedanganya umri wa baadhi ya wachezaji wake.
Nigeria wametilia mkazo kuwa hawana mchezaji yoyote aliye zaidi ya miaka 17 na kama ingekuwa hivyo tayari FIFA ingeshabaini kabla hata ya kuanza kwa michuano hiyo.
Kikosi cha Nigeria kina historia ya kutwaa kikombe hicho cha dunia kwa vijana mara 3.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni