MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sadick Mecky Sadick ameziomba
taasisi, kampuni na idara mbalimbali kujitokeza kudhamini mbio za Uhuru
Marathon zinazotarajiw akufanyika jijini Dar es Salaam Desemba 8, mwaka huu.
Mbali na hilo waandaaji pia wametuma mwaliko kwa wanariadha
mbalimbali maarufu duniania akiwemo Haile Gebre sellasie ili kumuomba ashiriki mbio
hizo.
Akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mbio hizo,
Sadick alisema, mbali na mialiko waliyotoa lakini mbio hizo ni muhimu zaidi kwaWatanzania
kwasasa kwani zina lengo la kudumisha amani, umoja na mshikamano uliopo miongoni
mwetu.
Kiongozi huyo ambaye ndiye Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi
alisema, katika kipindi hiki ambacho kuna baadhi ya watu wanataka kuvuruga amani,
umoja na mshikamano miongoni mwa wa Watanzania.
“Katika kipind hiki ambacho kuna baadhi ya watu wanafanya
hila za aina mbalimbali ili kutuvuruga ni vyema Watanzania wakazienzi mbio hizi
ambazo zimekuja katika wakati muafaka wa kudumisha yale yaliyoasisiwa na waasisi
wa taifa hili.
“Hivyo katika kipindi hiki ambacho tunatakiwa tudumishe
amani, umoja na mshikamano miongoni mwetu ni bora zaidi tukaona umuhimu wa mbio
hizi.
“Ni vyema pia nichukue nafasi hii kuzitaka kampuni,
taasisi na watu mbalimbali kuzidhamini mbio hizi ambazo ni zetu sote na zenye umuhimu
mkubwa kwa ustawi wa Taifa letu,” alisema Sadick.
Alifafanua kuwa, pale ambapo amani, umoja na mshikamano
unapokosekana miongoni mwa Taifa hakuna hata
mmoja atakayesalimika, hivyo ni jukumu la Watanzania wote kuitetea na kuilinda kwa
nguvu.
Alisema anajivunia Mkoa wa Dar es Salaam kuandaa mbio
hizo kwani jiji hilo lina umuhimu mkubwa wa kutangaza amani iliyopo ndani ya
Tanzania.
Kuhusu mbio alisema, kutakuwa na mbio ndefu za kilomita
42, kilomita 21 na kuna zile za kilomita 5 ambazo zitawahusisha watu wa kada mbalimbali,
wakiwemo mawaziri, wabunge, wanasiasa na za kilomita tatu zitakazo wahusu zaidi
viongozi wa ngazi za juu wa Serikali.
Katibu wa Kamati ya Maandalizi ya Uhuru Marathon,
Innocent Melleck alisema, wamealika wanariadha mbalimbali maarufu akiwemo Haile
Gebreselassie wa Ethiopia na wana imani kubwa anaweza kushiriki kama mambo
yataenda kama yalivyopangwa.
“Tumealika wanariadha mbalimbali maarufu na kama mipango
ikienda sawa tumemuomba pia mwanariadha maarufu duniani Haile Gebresellasie kuja
kushiriki katika mbio hizo,” alisema.
Mkurugenzi wa Michezo msaidi katikaWizara ya Habari,
Utamaduni, Vijanana Michezo, Juliana Yassoda alisema, anaimani kubwa mbio hizo pia
zitakuwa chachu kubwa ya kuinua mchezo huo hapa nchini.
“Sio kwa riadha
tu, kuna michezo mingi hapa nchini, lakini ni vyema vyama vya michezo hapa
nchini vikaweka mikakati na yotekelezeka ilikuhakikisha Tanzania inafanya vyema
zaidi,” alisema.
Mbioza Uhuru Marathon zinatarajiwa kufanyika kilaDesemba
8 ya kila mwaka hapa nchini.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni