MAONI YA
WANACHAMA YA KUUNDA KAMPUNI
Katika
Mkutano wa Kawaida wa Wanachama wa YANGA uliofanyika tarehe 16 Januari 2013
Mwenyekiti kwa niaba ya Kamati ya Utendaji aliwapa Wanachama wafikirie
mapendekezo ya YANGA kuwa Kampuni ama kutokuwa Kampuni kisha kuyawasilisha kwa
Katibu Mkuu wa YANGA.
Nachukua
nafasi hii kuwaambia Wanachama wa YANGA kuwa kuanzia leo tarehe 16 Oktoba 2013
mpaka tarehe 10 Novemba 2013, kutakuwa na sanduku moja (1) hapa Klabuni kwa
ajili ya kukusanya kura za maoni ya Wanachama ya kuanzisha Kampuni (NDIYO) au
kutokuwa Kampuni (HAPANA)
Kila
Mwanachama hai atakuwa na uhuru wa kupiga kura na atalazimika kuja na Kadi yake
ambapo itamzuia kupiga kura mara mbili au zaidi.
Zoezi
hili ni muhimu kwa ajili ya maendeleo ya YANGA.
“YANGA DAIMA MBELE NYUMA MWIKO”
Imetolewa na
LAWRENCE
MWALUSAKO
KAIMU
KATIBU MKUU
HABARI PICHA
![]() |
Kulia ni katibu mkuu Lawrence Mwalusako akiteta na afisa habari wa yanga Baraka Kizuguto |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni