TAARIFA KWA
VYOMBO VYA HABARI.
Mahakama ya Tanzania ni moja kati ya Mihimili mitatu ya Dola, na majukumu
yake makubwa kwa mujibu wa Katiba ni Kutafsiri sheria na kutolea maamuzi kesi
mbalimbali zinazoletwa Mahakamani.
107A:- (1) Sura ya
tano ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inasomeka kuwa:
‘Mamlaka yenye kauli
ya mwisho ya utoaji haki katika Jamhuri ya Muungano itakuwa ni Mahakama.’
Kufuatia jukumu hili
muhimu Mahakama imejiwekea dira ambayo ni; ‘Kutoa haki sawa kwa wote na kwa
wakati.’
Hata hivyo; Mahakama
ya Tanzania imekuwa ikikabiliwa na changamoto kadhaa likiwemo suala zima la
uendeshaji wa shughuli zake za kila siku.
Hata hivyo Mahakama
ya Tanzania,imefanikiwa kwa kiasi kikubwa, kufuatia hatua na michakato
mbalimbali ambayo tayari imekwishafanyika na mingine ikiwa kwenye hatua nzuri
yote yakiwa yanalenga katika kuboresha huduma ya utoaji haki nchini.
MAFANIKIO YALIYOFIKIWA
NA MAHAKAMA YA TANZANIA.
i.
Kurejewa kwa Muundo wa Mahakama na kuandaa Muundo
mpya wa Utawala wa Mahakama uliopitishwa katika Sheria mpya ya Uendeshaji
wa Mahakama (The Judicial Administration Act, No.4/2011). Kwa mujibu wa muundo
huu Shughuli za Kiutawala na za Kimahakama zimetenganishwa, Mhe. Msajili Mkuu
wa Mahakama ya Tanzania atasimamia shughuli za Mahakama tu, wakati Mtendaji
Mkuu (Chief Court Administrator) atashughulikia masuala ya Kiutawala.
Muundo huu mpya tayari umeanza kutekelezwa rasmi katika mwaka wa fedha
uliopita, 2012/2013. Hatua hii itaboresha na kuongeza ufanisi katika shughuli
za utoaji haki nchini.
Mchakato wa mabadiliko ya Muundo wa Mahakama ulianza miaka 16 iliyopita
kufuatia ripoti ya Kikosi kazi kilichoongozwa na Mhe. Jaji Mark Bomani ambayo
ilipendekeza kufanyika kwa mabadiliko ya Muundo wa Mahakama ili kuboresha
ufanisi katika utendaji kazi wa Mhimili huu muhimu.
ii.
Uanzishwaji wa Mfuko wa Mahakama chini ya Sheria ya
Uendeshaji wa Mahakama Na.4 ya mwaka 2011. Lengo la mfuko huu ni
kuwezesha uendeshaji wa mashauri katika Mahakama za ngazi zote kwa kuboresha
mfumo wa usikilizaji wa Mashauri katika Mahakama za ngazi zote kwa kuboresha
mfumo wa usikilizaji Mashauri na ununuzi wa vitendea kazi.
Kuanzishwa kwa Mfuko wa Mahakama kumesaidia
kuongezeka kwa bajeti ya Mahakama kutoka bilioni 20 kwa bajeti ya mwaka wa
fedha 2011/12 kuwa bilioni 30 kwa bajeti ya 2012/13 na kuwa bilioni 140 kwa
bajeti ya mwaka 2013/14.
Aidha, Mfuko umesaidia kuharakisha kasi ya usikilizaji wa mashauri na
idadi ya vikao vya Mahakama. Vikao vya Mahakama ya Rufani vimeongezeka kutoka
22 kwa mwaka wa fedha 2012/13 hadi 30 kwa mwaka huu wa fedha. Huku rufaa
zilizomalizika zikiongezeka kutoka 585 hadi 634 hadi kufikia mwezi wa Septemba
2013. Mahakama ya Rufani inakusudia kumaliza rufaa 1200 kwa mwaka 2014.
Mahakama Kuu yenye kanda 13 na inatarajia kumaliza mashuri 11000 wakati kwa
mwaka jana illimaliza mashauri 5600 na kutolea maamuzi mashauri. Mahakama Kuu
hadi kufikia mwezi Juni mwaka huu mahakama tayari ilikuwa imepokea mashauri
mapya 1402 na kumaliza mashauri 1781 kati ya hayo 936 akiwa ya jinai na 489.
yakiwa ya madai na yaliyobakia yakiwa ni mashauri ya jinai yaliko katika
masjala za kawaida.
Utaratibu huu pia umesaidia kuharakisha upatikanaji wa nakala za mwenendo
wa Mashauri na hukumu pamoja na kuwarahisishia kazi Majaji na mahakimu
wanaosikiliza kesi katika Mahakama hii. Mfuko huu pia utasaidia katika
kuboresha miundombinu ya Mahakama hususani Majengo, Vitendea kazi, maslahi ya
Watumishi n.k.
Mfuko umewezesha kufufuliwa kwa vikao vya kusukuma kesi na mashauri.
Vikao hivi ni muhimu kwani hukusanya wadau na kujadili mbinu za kupunguza
mashauri yenye muda mrefu mahakamani. Bajeti ya kuendesha vikao hivyo kwa ngazi
mbali mbali za mahakama imetengwa na tayari vikao hivyo vimeanza
kufanyika.
iii. Upatikanaji
wa fedha za O.C kadri ya Bajeti ilivyopangwa.
iv. Uanzishwaji
wa zoezi la nchi nzima la utunzaji bora wa kumbukumbu, ukusanyaji wa Takwimu na
matumizi yake na kuingiza mpango kamili wa matumizi ya TEHAMA kwenye shughuli.
v.
Kufanyika kwa vikao vya Mahakama ya Rufani na Mahakama Kuu (Court sessions kwa
asilimia 100).
vi. Kuanzisha
programu maalum ya uondoshaji wa mashauri ya muda mrefu Mahakamani.
vii. Kukamilishwa
kwa ujenzi wa jengo la Mahakama Kuu Bukoba na kuzinduliwa rasmi na Mhe. Rais
Jakaya M. Kikwete mnamo tarehe. 25, Julai, 2013.
viii. Uboreshwaji wa posho
za Wazee wa Baraza kutoka 1,500 hadi kufikia Shilingi 5000 kwa kila shauri
linalohitimishwa.
ix. Kuajiri
jumla ya Mahakimu 300 wahitimu wa Shahada ya kwanza ya Sheria na kuwasambaza
kwenye vituo vya Mahakama za Mwanzo katika wilaya 102. Hatua hii imesaidia
tatizo lililokuwepo la upungufu wa Mahakimu wa Mahakama za Mwanzo.
x.
Miradi ya ujenzi.
Aidha, Mahakama ya
Tanzania inaendelea na mchakato wa kuanza kwa ujenzi wa majengo ya Mahakama
katika ngazi mbalimbali.
· Ujenzi wa Makao Makuu ya
Mahakama ya Tanzania.
· Ujenzi wa Mahakama Kuu katika
Mikoa tisa; ambayo ni Mtwara, Kigoma, Mara, Lindi, Morogoro, Manyara, Singida,
Shinyanga na Dodoma.
· Kuanza kwa ujenzi wa Mahakama
ya Wilaya ya Bunda, Bariadi, Nkasi, Bukombe, Bagamoyo na Kilindi.
· Kuanza kwa ujenzi wa Mahakama
ya Mwanzo Buguruni, Kawe, Kigamboni, Makuyuni, Maili Moja, Songea, Mpanda,
Terrati, Mtowisa, Sangabuye, Ilolankulu, Mwanga, Mangaka, Makongolosi, Itigi,
Machame, Mkomazi, Gairo, Kiagata, Lukuledi na Longido; pamoja na ujenzi wa
Mahakama za Mwanzo Ngorongoro, Kolekero, Magoma na Bomang’ombe.
MIKAKATI YA
MAHAKAMA
· Dhamira ya Mahakama ni
kuondoa mashauri/kesi zote zenye umri zaidi ya miaka miwili (2).
· Kuboresha takwimu za
mashauri/ kesi zilizopo Mahakamani.
· Kuboresha na kusimamia
masjala.
· Kudhibiti kalenda za vikao
‘Court Sessions’.
· Kuweka “Benchmarks” kwa
maofisa wa Mahakama katika kumaliza mashauri kwa wakati.
· Kuboresha kanuni za kuendesha
mashauri.
· Kuimarisha utawala na
usimamizi wa mashauri.
Pamoja na Mafanikio
tajwa; jitihada za dhati bado zinaendelea kufanyika katika kuhakikisha kuwa
Mahakama inajengewa mazingira bora ya kufanyika kazi, kufanikisha jukumu la
Utoaji Haki kwa wakati nchini.
Asanteni kwa
kunisikiliza.
Contact; Mary Gwera.
(0756 866533/marygwerac@yahoo.com)
Afisa Habari
Mahakama ya Tanzania
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni