Kiungo wa Manchester City na timu ya taifa ya Ivory
Coast Yaya Toure ameteuliwa kuwa balozi wa amani wa program ya mazingira ya
umoja wa mataifa UNEP makao makuu yake yaliyopo Nairobi nchini Kenya.
Kiungo huyo mwenye miaka 30 ambaye ni mchezaji pekee
kutoka barani Afrika aliyopo katika orodha ya wachezaji 23 wanaowania tuzo ya
mchezaji bora wa mwaka ya FIFA anataraji kuungana wa timu ya wanaopinga
ujangili wa wanyama hususani tembo.
Yaya Toure baada ya kuteuliwa kwake amewataka
wanaAfrika kumuunga mkono na kushirikiana nae kutokomeza ujangili dhidi ya
viumbe hao.
Toure amesema kuwa timu yake ya taifa ya Ivory Coast
ilipewa jina la tembo wa Ivory Coast kutokana na uzuri wa wanaviumbe hao na
nguvu walizonazo na inawezekana ndani ya taifa lake bado kukawa na uhaba wa
wanaviumbe hao kutokana na ukatili wa baadhi ya watu wenye nia ya kufurahisha
matumbo yao pekee.
Uongozi wa UNEP umemtaka kiungo huyo mahiri barani
Afrika kupaza sauti yake, kutumia uwezo wake na jitihada zake kuelimisha jamii
kuacha biashara haramu inayokuza ujangili dhidi ya tembo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni