Hamad Yahya Juma wa Mtibwa Sugar
ndiye Mwenyekiti wa kwanza wa Bodi ya Ligi Tanzania (Tanzania Professional
League- TPL Board) baada ya kushinda katika uchaguzi uliofanyika jana mchana
(Oktoba 25 mwaka huu) kwenye ukumbi wa mikutano uliopo Golden Jubilee Tower, Dar
es Salaam.
Juma ambaye hakuwa na mpinzani
alipata kura zote kumi za ndiyo zilizopigwa na klabu za Ligi Kuu zilizohudhuria
mkutano huo. Klabu ambazo hazikuhudhuria uchaguzi huo ni JKT Ruvu, Mgambo
Shooting, Coastal Union na Rhino Rangers.
Naye Said Muhammad Said Abeid ambaye
pia hakuwa na mpinzani amechaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti kwa kupata kura zote
za ndiyo.
Kwa upande wa wajumbe wawili wa
Kamati ya Uendeshaji, wote Kazimoto Miraji Muzo wa Pamba na Khatib Omari
Mwindadi wa Mwadui wameshinda kwa kura zilizopigwa na klabu za Ligi Daraja la
Kwanza (FDL).
Muzo alipata kura 15 za ndiyo wakati
mbili zikimkataa, huku Mwindadi akipata kura 16 na moja ilimkataa. Klabu za FDL
ambazo hazikuhudhuria uchaguzi huo ni Transit Camp, Burkina Faso, Polisi Mara,
Stand United, Toto Africans, Polisi Tabora na Kanembwa JKT.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni