Jumamosi, 19 Oktoba 2013

DAR ES SALAAM DERBY SIMBA VS YANGA OCTOBER 20 TAIFA STADIUM


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI
JESHI LA POLISI TANZANIA
                                 

PRESS RELEASE
19/10/2013
JESHI LA POLISI KANDA MAALUM DSM LINAENDELEA NA MSAKO MKALI NA KUFANIKIWA KUKAMATA WATUHUMIWA 119 KWA MAKOSA MBALIMBALI.
·         KUKAMATWA WATUHUMIWA WAWILI WANAOMWAGIA WATU KEMIKALI AINA YA TINDIKALI

·         KUPATIKANA KWA SILAHA MBILI RIFFLE MOJA, BASTOLA MOJA,        RISASI TATU NA MTUHUMIWA MMOJA

·        KUKAMATWA KWA MAJAMBAZI WATATU AKIWEMO MWANAMKE WANAOKABA NA KUPORA PIKIPIKI

·         KUKAMATWA KWA WAHAMIAJI HARAMU KUMI NA SABA WA SOMALIA NA ETHIOPIA

·         KUKAMATWA KWA MATAPELI WATATU MMOJA AKIWA NA KITAMBULISHO BANDIA CHA IDARA YA USALAMA WA TAIFA

·         KUKAMATWA KWA WATUHUMIWA (91), BHANGI, KETE (183),
PULI (34), MISOKOTO (107) NA GONGO LITA (91)
·         RAI MMOJA RAIA WA SOMALI AKAMATWA NA NYARAKA ZA                                                SERIKALI
·         POLISI KUIMARISHA ULINZI MKALI WAKATI WA MECHI YA LIGI KUU YA  VODACOM  KATI YA SIMBA NA YANGA  UTAKAOFANYIKA TAREHE                                     20/10/2013
KUKAMATWA WATUHUMIWA WAWILI WANAOMWAGIA WATU KEMIKALI AINA YA TINDIKALI.
   Jeshi la Polisi Kanda Maalum  Dsm, mnamo tarehe 10/10/2013 majira ya saa mbili asubuhi huko maeneo ya Lumumba kariakoo lilifanikiwa kuwakamata watuhumiwa wawili wanaomwagia watu kemikali aina ya tindikali, ufuatiliaji huo ulifanywa kwa njia ya mtandao(Electronic Intelligence Analysis) na kuweza kuwabaini watuhumiwa hao.
    katika siku za hivi karibuni kumeibuka tabia ya matukio ya watu kumwagiwa kemikali aina ya tindikali DSM, Zanzibar na Arusha. Aidha watuhumiwa hao katika mahojiano ya awali walikiri kuhusika na tukio moja la kummwagia tindikali mfanyabiashara raia wa LEBANON aitwaye ALLY S/O IBRAHIMU FARHAT (33) Mkazi wa Upanga tukio ambalo liliripotiwa kituo cha Polisi Msimbazi MS/IR/7917/2012.
  Aidha taarifa za kiintelijensia zinaonyesha mbinu zilizotumika katika tukio hilo zinawiana na tukio la kumwagiwa sumu aina tindikali kwa mfanyabiashara aitwaye SAID S/O MOHAMED@SAAD(42), mkazi wa Mikocheni maeneo ya Msasani katika jengo la Msasani City Mall karibu na ubalozi wa marekani, ambaye ni mkurugenzi wa kampuni ya Home Shopping Centre jijini Dsm. Tukio liliripotiwa Kituo cha Polisi Oysterbay Mwezi wa saba mwaka 2013, OB/IR/7035/2013.
Mahojiano yanaendelea ili kubaini ushiriki wao katika tukio tajwa pamoja na kushirikiana na Zanzibar na mikoa mingine ili kubaini matukio mengine.



KUPATIKANA KWA SILAHA MBILI RIFFLE MOJA, BASTOLA  MOJA RISASI TATU NA MTUHUMIWA MMOJA
         Jeshi la Polisi kanda maalum Dsm mnamo tarehe 6/9/2013 majira ya saa sita kamili mchana huko maeneo ya Tandika Magorofani (W) Temeke askari wakiwa doria walifanikiwa kupata silaha moja bastola aina ya Browning AL.9 ikiwa na risasi tatu ndani ya magazine. –Awali askari walikuwa doria katika maeneo hayo na kuitilia mashaka pikipiki moja aina ya Boxer rangi nyekundu ambayo haikusomeka namba ikiwa na watu wawili, na pindi watu hao waliposimamishwa hawakutii amri ya kusimama na badala yake waliongeza mwendo, Na ndipo walipofika maeneo ya mtaa wa Bububu abiria aliyekuwa nyuma alidondosha mfuko mmoja wa plastiki ambao baada ya askari kuupekua walikuta silaha hiyo, Msako mkali unaendelea wa kuwatafuta watu hao wanaosadikiwa kuwa ni majambazi.
Katika tukio lingine mnamo tarehe 8/9/2013 majira ya saa kumi na moja jioni maeneo ya Yombo Dovya CCM(w) Temeke, Jeshi la Polisi kanda maalum lilifanikiwa kumkamata mtuhumiwa mmoja MFAUME s/o SAID (24) mkazi wa Mtwara akiwa na silaha moja aina ya Riffle yenye namba 181531 akiimiliki kinyume cha sheria.Mtuhumiwa anaendelea kushikiliwa kwa mahojiano zaidi.
KUKAMATWA KWA MAJAMBAZI WATATU AKIWEMO MWANAMKE WANAOKABA NA KUPORA PIKIPIKI
  Jeshi la Polisi Kanda Maalum DSM mnamo tarehe 17/10/2013 saa moja na dakika arobaini huko maeneo ya Coco beach(w) Ilala, mlalamikaji Joseph s/o Kilian(24)mkazi wa kawe ukwamani  akiwa ameegesha pikipiki yake no.T178 CMC aina SANLG nyekundu  maeneo ya Coco beach walikuja watu watatu  akiwemo mwanamke mmoja na kukodi pikipiki yake ili awapeleke oysterbay shule, wakiwa njiani ghafla ilitokea pikipiki no.T 127 CJL aina ya SunLG nyekundu ikiwa na watu watatu abiria mmoja alimwambia asimame, ghafla abiria wa kike aliyekuwa amempakia alimkaba shingoni kwa kushirikiana na abiria wa pikipiki ya pili lakini dereva wa pikipiki hiyo alifanikiwa kuondondoka chini akiwa amechomoa ufunguo na remote hivyo wezi hao walishindwa kuiwasha pikipiki hiyo, wezi hao kuona hivyo waliamua kupanda pikipiki yao na dereva huyo kuona hivyo aliwasha pikipiki yake na kuanza kuwakimbiza akiwa njiani aliomba msaada kwa dereva wa gari ndogo Toyota Allex na kumsaidia kuwafukuza wezi hao,  walipofika maeneo ya Palm Beach gari hiyo ilifanikiwa kuwagonga kwa nyuma na wao kuanguka chini na Polisi walipata taarifa ya tukio hilo wakishirikiana na polisi jamii waliokuwa karibu na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa 3 ambao ni: 1.Ramadhani s/o Saidi (20) mkazi wa Mbagala Saku,2.Maulidi s/o Ridhiwani (20) mkazi wa Mbagala Charambe,3.Siwema d/o ally (20) mkazi wa Tandika Kichangani, Watuhumiwa wanashikiliwa kituo cha Polisi Salender Bridge kwa mahojiano mara upelelezi utakapokamilika watapelekwa mahakamani.
KUKAMATWA KWA WAHAMIAJI HARAMU KUMI NA SABA WA                                   SOMALIA NA ETHIOPIA
     Jeshi la Polisi kanda maalum Dsm mnamo tarehe 6/09/2013 majira ya saa tano na nusu asubuhi huko maeneo ya Kipunguni ‘A’ katika msako endelevu wa kuwatafuta wahamiaji haramu wanaoishi nchini bila vibali Polisi wakiwa doria walifanikiwa kuwakamata watu saba ambao ni raia wa Somalia wanaoishi nchini kinyume na taratibu za kisheria.Watu hao ni 1.KURUMIE s/o ABDALLAH (28) msomali na mkazi wa Kariakoo, 2.FARAGH s/o ISACK (22) msomali mkazi wa Kariakoo 3.SAHLAL  s/o ABDI (34) msomali mkazi wa Kipunguni ‘A’ 4.MOHAMED s/o MAHMUD (42) msomali mkazi wa Gongo la Mboto, 5.FARAGHA N s/o DAHIR (22) msomali mkazi wa Kawe Beach,6.ABDULKADIR  s/o HASSAN (21) msomali mkazi wa Kipunguni ‘A’,7.MOHAMED s/o MUHAMED (21) msomali mkazi wa Kipunguni ‘A’ watu hao watakabidhiwa idara ya uhamiaji kwa hatua zaidi za kisheria. 
 Katika tukio lingine Jeshi la Polisi kanda maalum Dsm mnamo tarehe 8/10/2013 majira ya saa moja asubuhi huko maeneo ya Changanyikeni askari wakiwa katika doria walifanikiwa kuwakamata watu kumi ambao ni raia wa Ethiopia wanaoishi nchini bila kibali kinyume na taratibu za kisheria.Watuhumiwa hao ni 1.ELAMU s/o ABDUL (23), 2.EBEBE s/o GEBREMIKAL (32), 3.DINKAYO s/o DETAMO (30), 4.DESTA s/o SHANDE (25), 5.TUMISIDO s/o BASORE (20), 6.KESEYE s/o SHIGUTE (29), 7.DANIEL s/o LANDABO (25), 8.TSIGAYE s/o TADESA (25), 9.BIRIHANI s/o MACHULA (22), 10.BEKELE s/o CHUFAMO (25). Watuhumiwa hao wote wanaendelea kuhojiwa ili kubaini watu wanaofanya biashara hiyo haramu ya kuwasafirisha pamoja na msako mkali  wa  kuwabaini  whamiaji wengine wote wanaoishi nchini bila vibali maalum ili sheria ifuate mkondo wake.

KUKAMATWA KWA MATAPELI WATATU MMOJA AKIWA NA KITAMBULISHO BANDIA CHA IDARA YA USALAMA WA TAIFA
       Jeshi la Polisi kanda maalum Dsm mnamo tarehe 8/10/2013 saa mbili kamili usiku huko maeneo ya Beko hotel, Kawe Maringo askari katika ufuatiliaji wa tukio la kuleweshwa madawa kwa JACKLINE d/o GACHANGA (34) mfanyabiashara mkazi wa Salasala na hatimaye kuibiwa cheni moja ya dhahabu,pete moja ya dhahabu ,fedha taslimu TSHs 800,000/=,simu moja aina ya nokia pamoja na laptop moja,askari walifanikiwa kuwakamata watuhumiwa wawili ambao ni KENEDY s/o MAGIGE  SAMWEL (35) mkazi wa Tabata na TAKULA  s/o ABDALLAH (32) mkazi wa Mbezi Beach ambapo wote walitambuliwa na mlalamikaji  JACKLINE. Aidha mtuhumiwa KENEDY s/o MAGIGE alipopekuliwa alikutwa na kadi za benki za watu mbalimbali pamoja na kitambulisho bandia cha usalama wa taifa. Watuhumiwa walipohojiwa wote walimtaja mshiriki mwenzao KHALIFAN s/o MALEMA (37) mkazi wa Kimara ambapo askari usiku huo walifanikiwa kumkamata akiwa na mzani wa kupimia dhahabu.Watuhumiwa wote wanaendelea kushikiliwa na Polisi na pindi upelelezi utakapokamilika watafikishwa mahakamani.
KUKAMATWA KWA WATUHUMIWA (46), BHANGI, KETE (252), PULI (8), MISOKOTO (13) NA GONGO LITA (193)
       Jeshi la Polisi Kanda maalum Dsm limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa 46, bhangi  kete 252, bhangi puli 8,bhangi misokoto  13 na gongo lita 3 , katika operesheni  endelevu ya vita dhidi ya madawa ya kulevya  iliyoanza tangu 11.10.2013 hadi tarehe …  katika maeneo mbalimbali ya jiji la DSM. Watuhumiwa hao ni SAID S/O ABDALLAH  (40) ALLY S/O ABDALLAH (42), MUHIDI S/O HAMAD (22), MOUHAMED S/O OMAR (25), SELEMAN S/O SHABANI (33),SALUM S/O ISMAIL (25), SHABAN S/O OMAR (32), REHEMA D/O MUNGI (26), OMAR S/O MANDA (21), HEMED S/O ABDALLAH (20), FATUMA D/O MUOHAME (20), MAWAZO S/O JUMANNE (37), KUDRA D/O SAID  (41), YASIN S/O JAFAR (30), MOUHAMED S/O SALUM (26), ANGELBERT S/O DONARD (29),  SHARIZ S/O ALLY (18), JUMA S/O SAID (40),  pamoja na watuhumiwa wengine (85), watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani upelelezi utakapokamilika.
RAI MMOJA RAIA WA SOMALI AKAMATWA NA NYARAKA ZA                                           SERIKALI
    Jeshi la polisi kanda maalum DSM mnamo tarehe 18/10/2013 majira ya saa nne kamili usiku huko mwananyama A walifanikiwa kumkamata raia wa Somali aitwaye JAMALI S/O IBRAHIMU(42) ambaye alikuwa akiishi kwenye nyumba mmoja ya wageni iitwayo  MRANGI GUEST HOUSE, baada ya polisi kupata taarifa hizo walifuatilia na kumkamata mtuhumiwa huyo akiwa na nyaraka za serikali kama ifuatavyo;
1.Form no.130 za maombi ya makazi
2.Stakabadhi 21 za malipo ya vibali vya makazi
3.Nakala 8 za hati za kusafiria zenye picha za waombaji ambazo ni raia wa kisomali
4.Bahasha moja yenye picha mbalimbali za waombaji ambao ni raia wa kisomali.
     Aidha katika mahojiano mtuhumiwa anadai anaishi katika nyumba hiyo ya wageni kwa kipindi cha miaka mitatu, ambapo awali alikuwa akiishi kwa msomali mwenzake iliyopo mwananyamala ambapo imekwisha uzwa, kuhusu uhalali wake wa kuishi nchini, kibali alichokuwa nacho cha uhalali wa kuishi hapa nchini kimeisha muda wake tangu tarehe 08/08/2013 mahojiano zaidi yanaendelea ili kuweza kubaini mtandao mzima anaoutumia na kupata nyaraka hizo za wizara ya mambo ya ndani idara ya uhamiaji.

POLISI KUIMARISHA ULINZI MKALI WAKATI WA MECHI YA LIGI KUU YA  VODACOM  KATI YA SIMBA NA YANGA  UTAKAOFANYIKA TAREHE 20/10/2013
Jeshi la Polisi kanda maalum Dsm kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama tumejipanga ipasavyo kuhakikisha mchezo huo wenye mvuto mkubwa kwa mashabiki wa Tanzania, Nchi za Afrika Mashariki na Afrika nzima kuchezwa katika hali ya usalama.
Aidha tunaomba wananchi wasiwe na shaka yeyote ya kiusalama na pia watupe ushirikiano wa kutoa taarifa kwa jambo lolote watakaloliona kuwa linaweza kuwa chanzo cha uvunjifu wa amani kwa kipindi chote watakapokuwa nje au ndani ya uwanja.
Taarifa hizo zitafanyiwa kazi haraka na kuwachukulia hatua wale wote watakaokuwa wamehusika katika tukio husika kulingana na sheria za nchi/kanuni za usalama za shirikisho la soka duniani (FIFA Safety Guidelines).
Vile vile tunawasihi mashabiki wote wasije na vitu vyovyote ambavyo vinaweza kutumika kama sila silaha (mfano soda za chupa na makopo ya maji, vipande vya chuma, visu, mawe, au silaha za moto na vitu vya milipuko) vitu hivyo ni hatari pindi ikitokea vurugu na kinyume na kanuni za usalama za FIFA.
Aidha katika kuhakikisha watu wanaingia wakiwa salama tutafanya upekuzi katika milango yoye ya kuingilia kwa kutumia mashine za kisasa(Metal Detector)  na kuwachukulia hatua mashabiki watakaokiuka agizo hilo.
Kutakuwa na ulinzi katika majukwaa na askari na walinzi wasaidizi (stewards) wa kutosha katika majukwaa yote kuhakikisha usalama unakuwepo kwa kipindi chote. Tunawakumbusha mashabiki kuwa wastaarabu kwa kukaa majukwaaa yanayoendana na aina/thamani halisi ya tiketi walizokata na si kuvamia maeneo ya VIP. Pamoja na kuimarisha ulinzi wa ndani na nje ya uwanja (Inner and Outer Perimeter Security measures) tutatumia kamera  za CCTV  ili kufuatilia mienendo ya matukio yote.
Pia barabara ya uwanja wa Taifa itafungwa kwa muda ili kupunguza foleni zisizokuwa za lazima, pia magari hayataruhusiwa kuegeshwa katika eneo hilo na badala yake watakaopenda kuja na magari watafute maeneo mengine salama ya kuegesha magari yao.

S. H. KOVA – CP
KAMISHNA WA POLISI KANDA MAALUM
DAR ES SALAAM

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni