Alhamisi, 31 Oktoba 2013

HAKUNA ZAIDI YA MIAKA 17 HAPA




Shirikisho la mpira wa miguu la Nigeria limesisitiza kuwa hakuna mchezaji yoyote kati ya wachezaji 21 wanaoiwakilisha nchi hiyo kwenye michuano ya kombe la dunia kwa vijana chini ya miaka 17 aliyevuka umri huo.
Msisitizo wa shirikisho hilo umekuja siku moja baada ya kutuhumiwa kuwa wamechanganya kikosi hicho na wachezaji waliovuka miaka 17 na ndiyo maana wamekuwa wakipata ushindi mnono tofauti na timu zingine.
Kikosi cha Nigeria kiliibanjua Iran magoli 4-1 katika raundi ya 16 ya michuano hiyo matokeo ambayo yamezua maneno kuwa kikosi hicho kimedanganya umri wa baadhi ya wachezaji wake.
Nigeria wametilia mkazo kuwa hawana mchezaji yoyote aliye zaidi ya miaka 17 na kama ingekuwa hivyo tayari FIFA ingeshabaini kabla hata ya kuanza kwa michuano hiyo.
Kikosi cha Nigeria kina historia ya kutwaa kikombe hicho cha dunia kwa vijana mara 3.

MAPUNDA : SASA NARUDI NYUMBANI



 
Mlinda mlango wa mabingwa wapya wa ligi kuu soka ya nchini Kenya Gor Mahia Ivo Philip Mapunda,amesema kuwa kila kitu kinawezekana kwasasa baada ya kupata nafasi kurejea kwenye timu yake ya Taifa ya Tanzania bara baada ya kuwa nje kwa muda mrefu.
Kipa huyo kujumuishwa kwenye timu ya taifa ya Tanzania bara The Kilimanjaro Stars ambayo inajiandaa na michuano ya Chalenj itakayofanyika nchini Kenya kumezua mshangao mkubwa miongoni mwa mashabiki mbalimbali wa soka waliopo Kenya na Tanzania.
Mapunda ambaye ni mahiri kupangua mikwaju ya penalty amejumuishwa katika kikosi cha wachezaji 30 ambao watafanyiwa mchujo na kubakia wachezaji 10 watakaoungana na kikosi cha kwanza cha The Kilimanjaro Stars.
Mapunda amesema haijalishi yeye kuitwa kikosi cha kwanza au cha pili kikubwa ni kuonekana kwenye kikosi hicho ambacho kwa muda mrefu hajakitumikia na ameahidi kufanya jitihada zake kuhakikisha wanarejea na kikombe nyumbani Tanzania.
Michuano ya Chalenj inataraji kutimua vumbi kuanzia Novemba 27 hadi Disemba 12 mwaka huu na kipa huyo tegemezi wa Gor Mahia ataungana na makipa wengine akiwemo Aishi Manula kutoka Azam na Hussein Sharif kutoka Mtibwa katika kikosi kitakachofanyiwa na mchujo kabla ya kuungana na mlinda mlango namba moja wa Yanga Afrika Ally Mustapha Mtinge Barthez katika kikosi kamili kitakacho kwea pipa kuelekea Nairobi nchini Kenya.

Jumatano, 30 Oktoba 2013

ERNIE BRANDS AWAPOZA MASHABIKI WA DAR YOUNG AFRICANS



Jamani tulieni waacheni vijana wangu
Kocha mkuu wa mabingwa watetezi wa ligi kuu soka ya Tanzania bara Yanga Afrika Ernie Brands amewatuliza mashabiki wa Yanga na kuwataka kuacha kuwashutumu baadhi ya wachezaji kuwa wanatumiwa kwa namna moja ama nyingine kuihujumu timu hiyo.
Kauli ya Brands imekuja baada ya  kusikitishwa na kauli za baadhi ya mashabiki wa Yanga waliojitokeza jana uwanja wa Taifa Dar es Salaam wakati wa mchezo wao uliomalizika kwa Yanga kuondoka na alama 3 baada ya kuwabanjua Mgambo JKT magoli 3-0.
Baadhi ya mashabiki wa Yanga walionekana kuendelea kumlaumu mlinda mlango namba moja wa Yanga Ally Mustapha Mtinge Barthez pamoja na nahodha wao Nadir Haroub Ally Canavaro kwa kile wanachokidai walipokea mpunga na kusababisha kutoka sare na watani wao wa jadi wekundu wa msimbazi Simba.
 Brands amesema kuwa hayo yote ni matokeo ya mchezo na wala mashabiki hawapaswi kumlaumu mtu yoyote na badala yake waunge mkono juhudi zinazofanywa na wachezaji wao za kuhakikisha wanatetea ubingwa msimu huu wa ligi.
 They have to support us and not blaming goalkeeper, if someone made a mistake they have to help us and support us in good times and bad times”
 Nae Dakatari mkuu wa Yanga Afrika Nassor Ally Matuzya akafunguka kuhusiana na majeruhi waliopo kikosini hapo na endapo kutakuwa na uwezekano wa kuwa na kikosi chote kamili kuelekea katika mchezo huo dhidi ya JKT Ruvu.
“Kikosi kinaendelea vizuri, tuna majeruhi wachache akiwemo Nizar Khalfani ana majeruhi ya paja kwa nyuma, yupo David Luhende ambaye pia nae anasumbuliwa na paja, Nizar aliumia mazoezini wakati Luhende aliumia wakati wa mechi iliyopita dhidi ya Rhino Rangers”.
“Tunae pia majeruhi Juma Abdul ambaye aliumia mechi iliyopita pamoja na Abdallah Mghui Messi timu inaendelea vizuri na wengine wote wanaendelea na maandalizi”.

RAGE AMFUNGIA MILANGO JUMA KASEJA



Toka huna chako hapa ole wako urudi
Mabingwa wa zamani wa ligi kuu wekundu wa msimbazi Simba hawatarajii kumrejesha kikosini aliyekuwa mlinda mlango wao namba moja Juma K Juma(Juma Kaseja)  walitemana nae mwishoni mwa msimu uliopita.
Mwenyekiti wa wekundu hao Ismail Aden Rage amesema kuwa suala la Kaseja litabaki kuwa historian a wala hawafikirii kumrejesha tena kipa huyo kwakuwa tayari wanae kipa chaguo lao Mganda Abel Dhaira.
Rage amesema kuwa maneno yanayozungumzwa na kuandikwa kwenye baadhi ya vyombo vya habari kuwa Kaseja atarudi Simba ni ya uchochezi na yana lenga kuwavuruga tu.
Dah jamani hamnionei hata huruma?
“Hii habari ya Kaseja karudi Simba inawasaidia nini wanasimba?tuko kwenye premier League ni kutaka kuwavuruga wanasimba waache kuconcentrate kwenye mambo yao, dirisha dogo bado, usajili bado aliyekwambieni tunabadilisha golikipa nani.”
Hakatiw mtu hapa
Tuandike vitu ambavyo vinatusaidia kuleta maendeleo, kila siku mnaandika habari za uwongo yanga kafanya hivi simba kafanya hivi”.

YAYA TOURE NAMED UN AMBASSADOR



Kiungo wa Manchester City na timu ya taifa ya Ivory Coast Yaya Toure ameteuliwa kuwa balozi wa amani wa program ya mazingira ya umoja wa mataifa UNEP makao makuu yake yaliyopo Nairobi nchini Kenya.
Kiungo huyo mwenye miaka 30 ambaye ni mchezaji pekee kutoka barani Afrika aliyopo katika orodha ya wachezaji 23 wanaowania tuzo ya mchezaji bora wa mwaka ya FIFA anataraji kuungana wa timu ya wanaopinga ujangili wa wanyama hususani tembo.
Yaya Toure baada ya kuteuliwa kwake amewataka wanaAfrika kumuunga mkono na kushirikiana nae kutokomeza ujangili dhidi ya viumbe hao.
Toure amesema kuwa timu yake ya taifa ya Ivory Coast ilipewa jina la tembo wa Ivory Coast kutokana na uzuri wa wanaviumbe hao na nguvu walizonazo na inawezekana ndani ya taifa lake bado kukawa na uhaba wa wanaviumbe hao kutokana na ukatili wa baadhi ya watu wenye nia ya kufurahisha matumbo yao pekee.
Uongozi wa UNEP umemtaka kiungo huyo mahiri barani Afrika kupaza sauti yake, kutumia uwezo wake na jitihada zake kuelimisha jamii kuacha biashara haramu inayokuza ujangili dhidi ya tembo.