Jeshi la polisi kanda maalumu ya Dar es Salaam
inawashikilia watu watatu kwa kosa la kufanya vurugu wakati wa mchezo wa ligi
kuu soka ya Tanzania bara kati ya wekundu wa msimbazi Simba dhidi ya Kagera
Sugar mwanzoni mwa juma lililopita, mchezo uliomalizika kwa mabomu ya machozi
kupigwa baada ya timu hizo kwenda sare ya kufungana bao 1-1.
Kamishna wa polisi kanda maalumu ya Dar es Salaam
Suleimani Kova amesema kuwa watu hao watafikishwa mahakamani wakati wowote
kutoka sasa nab ado wanaendelea na msako kuwabaini wengine ambao pia wamehusika
katika vurugu hizo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni