Timu za Taifa za Future Taifa Stars na Taifa Stars
zinacheza kesho (Novemba 13 mwaka huu). Mechi hiyo ya kirafiki itafanyika
Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume jijini Dar es Salaam kuanzia saa 10 kamili
jioni.
Mechi hiyo ni maalumu kwa Benchi la Ufundi la Taifa
Stars linaloongozwa na Kim Poulsen kuangalia wachezaji kumi kutoka Future Taifa
Stars watakaoongezwa katika Taifa Stars tayari kwa mechi ya kirafiki ya
kimataifa itakayochezwa Novemba 19 mwaka huu jijini Arusha.
Watazamaji 300 tu wataruhusiwa kushuhudia mechi hiyo
kwa kiingilio cha sh. 5,000.
Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium
Lager imeingia kambini leo (Novemba 12 mwaka huu). Miongoni mwa wachezaji
wanaotarajia kuripoti ni kipa Ivo Mapunda wa Gor Mahia.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni