Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF),
Jamal Malinzi atafungua rasmi michuano ya vijana wenye umri wa chini ya miaka
20 (U20) kwa klabu za Ligi Kuu ya Vodacom mwaka huu.
Uzinduzi wa mashindano hayo utafanyika kesho
(Novemba 17 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam saa
2 kamili asubuhi. Mechi ya ufunguzi itakuwa ya kundi A kati ya Azam na Coastal
Union.
Mechi nyingine za kesho ni kundi; Yanga na Mbeya City
(saa 8 mchana- Uwanja wa Karume), kundi B ni Ruvu Shooting na Ashanti United
(saa 4 asubuhi- Uwanja wa Karume), Oljoro JKT na Simba (saa 10 jioni- Uwanja wa
Karume).
Kundi C kutakuwa na mechi kati ya Kagera Sugar na
Mtibwa Sugar itakayochezwa saa 2 kamili asubuhi kwenye Uwanja wa Azam Complex,
na kwenye uwanja huo huo saa 10 jioni ni Rhino Rangers dhidi ya Tanzania
Prisons.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni