Nigeria wameandika rekodi mpya ya kutwaa kikombe cha
dunia kwa vijana chini ya maiaka 17 kwa mara ya nne hapo jana wakiwatandika
mabingwa watetezi Mexico magoli 3-0.
Mbali na kikombe hicho hicho kikosi cha Naigeria
kimezawadia tuzo nyingine ya kuwa timu iliyoonesha nidhamu ya hali ya juu
pamoja na kutwaa zawadi ya kuwa na mlinda mlango bora.
Katika michuano ya mwaka huu iliyounguruma katika
nchi za falme za kiarabu, kikosi cha Niageria kimeshuka dimbani mara 7,
kimeshinda michezo 6, kimetoka sare mchezo 1, na kikiwa hakijapoteza mchezo
mmoja pamoja na mambo mengine kimefanikiwa kutikisa nyavu mara 26 huku
wakiruhusu nyavu zao kutikiswa mara 5 pekee.
Rekodi ya kikosi cha Nigeria kutwaa kombe la dunia
kwa vijana ilianza kuandikwa mwaka 1985, ikafuatiwa mwaka 1993, na baadae 2007
kabla ya jana kuongeza rekodi nyingine.
Kikosi hicho pia kimewahi kumaliza kwenye nafasi ya
pili kwa mara tatu tofauti, kama itakumbukwa mwaka 1987, 2001 na 2009.
Mwaka 2013 unakuwa mwaka wenye mafanikio makubwa kwa
wanaigeria wakifanikiwa kutwaa vikombe viwili vikubwa, kikiwemo cha AFCON
ambacho timu ya taifa ya wakubwa kilitwaa mapema mwaka huu wakati timu ya
vijana ikitwaa kikombe cha dunia hapo jana.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni