Jumatatu, 11 Novemba 2013

AL AHLY YAFANIKIWA KUTETEA KIKOMBE CHAKE



 Ligi ya mabingwa barani Afrika ambapo jana kumepigwa fainali ya pili, ikishuhudiwa Al Ahly ya nchini Misri ikifanikiwa kutetea kikombe chake baada ya kuwachapa Orlando Pirates kutoka Afrika kusini magoli 2-0.

Ahly, imeandika historia nyingine jana ikibeba taji la ubingwa wa Afrika kwa mara ya nane ikiwa imeshinda ushindi wa jumla magoli 3-1, magoli mawili kwenye mchezo huo wa hapo jana pamoja na ile sare ya bao 1-1 katika mchezo wa fainali ya kwanza iliyopigwa huko Soweto Afrika kusini.

 Shukrani za pekee katika ushindi huo wa magoli mawili umuendee mkongwe Mohammed Abutrika aliyetikisa nyavu dakika ya 54 pamoja na Ahmed AbdulZahir dakika ya 78.

Kikosi hicho kimezawadiwa dola za kimarekani Millioni 1-5 na wanataraji kuliwakilisha bara la Afrika kwenye michuano ya kombe la dunia la vilabu itkayopigwa kuanzia Disemba 11 hadi Disemba 21 mwaka huu nchini Morocco.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni