Jumatatu, 4 Novemba 2013

MBEYA CITY KUTUA DAR KWA NDEGE

Wakali wa jiji la Mbeya timu ya Mbeya City inataraji kutua Dar saa chache kabla ya mchezo wao dhidi wa waoka mikate wa Azam Fc.
Mbeya City watashuka simbani Alhamis ya Novemba 07 kwenye uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam kupapatuana na waoka mikate wa Azam Fc.
Kwa mujibu wa msemaji wa Mbeya City Saleh Kupaza amesema kuwa lengo lao ni kuendeleza ushindi hivyo wanahitaji muda wa kutosha kukaa chimbo kabla ya kuja Dar kusaka alama tatu mbele ya Azam Fc.
Mbeya City itashuka dimbani ikiwa na kumbukumbu ya kushinda mchezo uliopita dhidi ya Ashanti United halikadhalika kwa Azam Fc wenyewe.
Kimenukaaaaaa


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni