Tayari orodha ya wachezaji watano wanaowania tuzo ya
mwanasoka bora wa Afrika imekiwshatolewa, kiungo wa Ivory Coast Yaya Toure
aking’ara kwa mara ya tano mfululizo, mshindi akitaraji kutangazwa jumatatu ya
Disemba 2 mwaka huu.
Washiriki wengine wanaowania tuzo hiyo ni nyota wa Nigeria Victor Moses na John Mikel
Obi, Piere Emerick Ubamiyang kutoka Gabon naJonathan Pitroipa kutoka Burkina
Faso.
Mashabiki wa soka barani Afrika wamepewa nafasi ya
kumpigia kura mchezaji wampendae kwa kuandika namba yake ya kushiriki, Andika
namba 1 kumpigia kura Ubamiyang, namba 2 kumpigia kura Victor Moses, namba 3 kumchagua
Mikel, namba 4 kumchagua Jonathan na namba 5 kumchagua Yaya Toure kisha unatuma
kwenda namba 44 7786 29 20 08 ukianzia na namba ya kujumlisha.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni