Jumatatu, 11 Novemba 2013

ETHIOPIA KUTUA NIGERIA NOVEMBER 14

Timu ya taifa ya Ethiopia wanataraji kukwea pipa alhamis hii kuelekea Calabar kukamilisha kibarua chao cha mtoano mchujo wa kuomb la dunia dhidi ya timu ya taifa ya Nigeria The Super Eagles.

Shirikisho la mpira wa miguu la Ethiopia limesema kuwa wataondoka kuelekea Calabar wakiwa na mashabiki ili kukipa hamasa kikosi chao kuelekea katika mchezo huo muhimu kwa taifa lao, na tayari msafara wa awali wa kikosi hicho umeshawasili huko Nigeria ukiongozwa na katibu mkuu wa shirikisho kuhakikisha kila kitu kinakuwa sawa kabla ya mchezo wa hapo jumammosi.

Ethiopia walipoteza mchezo uliopita kwa magoli 2-1 dhidi ya Nigeria mchezo uliopitwa Adis Ababa nchini humo na sasa wanahitaji ushindi wa magoli 2-0 kujihakikishia tiketi ya kushiriki fainali hizo mwakani nchini Brazil.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni