Jumatatu, 4 Novemba 2013

KOMBE LA DUNIA KUTUA BONGO




Contacts for Media:                                                                               
Maurice Njowoka                                                                       Gerald Ndalahwa Ndimila
Brand Manager Tanzania                                                           PR Manager
Coca-Cola Central, East & West Africa Ltd                                Sonda Communications               
Cell: 0688341201                                                                Tel: +255783188181
mnjowoka@coca-cola.com                                               gerald@sondacom.co.tz

TANZANIA KUWA MWENYEJI WA ZIARA YA KOMBE HALISI LA FIFA LA DUNIA 29/30 NOVEMBA, 2013

“Ziara ya Kombe la FIFA la Dunia na Coca-Cola” Kuwasili Dar es Salaam Novemba 29 ikiwa ni sehemu ya ziara ya dunia

Coca-Cola kugawa tiketi bure kwa mashabiki wa soka jijini Dar es Salaam ili kuwapa fursa ya kushuhudia Kombe halisi la FIFA la Dunia

Dar es Salaam, Jumatatu, Novemba 4, 2013 … Kombe la FIFA la Dunia – kielelezo halisi na nembo ya ubora wa soka duniani – litawasili jijini Dar es Salaam tarehe 29 Novemba mwaka huu wa 2013.

Coca-Cola inalifanya Kombe la FIFA la Dunia 2014, kuwa karibu zaidi na mashabiki wa soka na tukio kubwa kuliko fainali nyingine zilizopita. Ziara ya Kombe la FIFA la Dunia na Coca-Cola litatoa fursa kwa mashabiki zaidi ya milioni moja kushuhudia kombe halisi la FIFA la Dunia katika nchi zao.

Hii ni ziara kubwa na ndefu zaidi ya kombe la dunia. Ni ziara ya nchi 88 inayodumu kwa muda wa miezi tisa ambayo itajumuisha nchi 39 za bara la Latin Amerika ambako ndio bara mwenyeji wa fainali za kombe la dunia 2014 ilipo. Vile vile ziara hii itajumuisha nchi 50 ambazo hazijapata fursa ya kuwa wenyeji wa ziara ya kombe la dunia.

Ziara ya kombe la dunia imeanzishwa kutokana na ushirikiano wa aina ya pekee uliopo kati ya FIFA na Coca-Cola.  Kampuni ya Coca-Cola ni mshirika wa FIFA wa hali ya juu na ni moja ya washirika wa FIFA wa muda mrefu.

Akiongea wakati wa hafla rasmi ya kutanganza ujio wa kombe la FIFA la Dunia nchini Tanzania, Meneja Mkazi wa Coca-Cola Tanzania Yebeltal Getachew alisema kwamba ziara ya kombe la dunia itatoa wasaa adimu kwa maelfu ya wapenzi wa soka jijini Dar es Salaam kuliona kwa karibu kombe halisi la dhahabu la FIFA la Dunia.  “Kupitia ziara hii na promosheni nyingine kuelekea fainali za kombe la FIFA la Dunia 2014, Coca-Cola itasheherekea hamasa ya soka na kujalibu kuzifanya fainali zijazo kuwa shirikishi zaidi kuliko zilizopita,” alisema.

Wakati wa ziara ya kombe la dunia, mashabiki watapata nafasi ya kufurahi na kuliona kombe halisi la FIFA la Dunia kwa karibu. Tiketi zitatolewa na Coca-Cola kupitia promotioni mbalimbali. 

Mashabiki pia watapata fursa ya kupiga picha na kombe, kutazama video inayoonyesha matukio mbalimbali ya kihistoria ya kombe la FIFA la Dunia na kufurahia burudani za kusisimua. 

Ziara ya Kombe la FIFA la Dunia 2013 limezingatia mafanikio makubwa ya ziara ya kombe hilo zilizofanyika mwaka 2006 na 2009 ambapo mamilioni ya wapenzi wa soka walipata nafasi ya kuliona kwa karibu kombe hilo ambalo ni zawadi ya thamani zaidi ya mpira wa miguu duniani.

Kombe la FIFA la Dunia huzawadiwa timu inayoshinda fainali za kombe la dunia.  Kombe hilo lina urefu wa sentimita 36.8 (14.5 inches), uzito wa gramu 6,175 (13.61 poundi) na limetengenezwa kwa dhahabu tupu (18-carat gold).  Timu bingwa hushikilia kombe hilo hadi fainali zinazofuata, baada ya hapo hupewa mfano wake mbalo siyo la dhahabu.  Chini ya kombe hilo kuna kina leya mbili za malachite, wakati kitako chake kinaonyesha washindi wa kombe la dunia tangu 1974.

Kampuni ya Coca-Cola ni moja ya washirika wa muda mrefu wa FIFA, na ushirikiano huo ulikuwa rasmi mwaka 1974 na kuwa mdhamini rasmi wa kombe la FIFA la Dunia mwaka 1978.  Coca-Cola ilianza kuweka matangazo yake kwenye viwanja vya Kombe la FIFA la Dunia tangu. Mwezi Novemba 2005, Coca-Cola na FIFA waliongeza muda wa ushirkiano wao. Ushirikiano huo unaongezwa kuzingatia masharti fulani fulani hadi 2022.

Ikiwa mshirika wa FIFA wa vinywaji baridi, Kampuni ya Coca-Cola imepewa haki za udhamini katika mashindano yote ya FIFA, ikiwa ni pamoja na Kombe la FIFA la Dunia na haki pekee za kujitangaza.

Ziara ya kombe la dunia inakuja kufuatia matukio makubwa ya kimichezo ambayo Coca-Cola iliyafanya kuelekea kuelekea fainali za kombe la FIFA la Dunia, ikiwa ni pamoja na mashindano ya vijana chini ya umri wa miaka 15 ya Copa Coca-Cola yaliyomalizika hivi karibuni.
                                               
MWISHO
Meneja Mkazi wa Coca-Cola Yebeltal Getachew akitangaza ujio wa Kombe la FIFA la Dunia nchini Tanzania Novemba 29, 2013. Kushoto ni Mkurugenzi wa michezo nchini Bw. Leonard Thadeo.  
Mkurungezi wa michezo nchini Bw. Leonard Thadeo akielezea faida ambazo Tanzania itazipata kutokana na ujio wa Kombe la FIFA la Dunia. Kombe hilo ambalo ni kielelezo cha ubora wa soka dunia litawasili jijini Dar es Salaam Novemba 29, 2013.
Meneja Bidhaa wa Coca-Cola Tanzania Maurice Njowoka akiongea na waandishi wa habari wakati wa hafla ya kutangaza ujio wa Kombe la FIFA la Dunia nchini Tanzania. Kombe hilo litawasili jijini Dar es Salaam Novemba 29, 2013.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni